Hashd al Shaabi: Marekani inataka kumalizia hamaki zake kwetu
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i61891-hashd_al_shaabi_marekani_inataka_kumalizia_hamaki_zake_kwetu
Kamanda wa harakati ya kujitolea ya wananchi wa Iraq maarufu kwa jina la al Hashd al Shaabi amesema kuwa, Marekani bado imejawa na hamaki na inataka kumalizia hamaki zake hizo kwa harakati hiyo ya wananchi ambayo inavuruga njama za Wamarekani hasa baada ya harakati hiyo kulishinda genge la kigaidi la Daesh (ISIS) lililoundwa na Marekani.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jun 29, 2020 08:07 UTC
  • Hashd al Shaabi: Marekani inataka kumalizia hamaki zake kwetu

Kamanda wa harakati ya kujitolea ya wananchi wa Iraq maarufu kwa jina la al Hashd al Shaabi amesema kuwa, Marekani bado imejawa na hamaki na inataka kumalizia hamaki zake hizo kwa harakati hiyo ya wananchi ambayo inavuruga njama za Wamarekani hasa baada ya harakati hiyo kulishinda genge la kigaidi la Daesh (ISIS) lililoundwa na Marekani.

Shirika la habari la FARS limemnukuu Ali al Husaini, mmoja wa makamanda wa ngazi za juu wa harakati ya al Hashd al Shaabi huko Iraq akisema, baadhi ya nchi za Magharibi na za Kiarabu zinaeneza fitna na zinafanya propaganda kubwa dhidi ya harakati hiyo kutokana na ushawishi na nguvu zake kati ya wananchi wa Iraq na kutokana na kufanikiwa kwake kusambaratisha njama za maadui wa Iraq za kutumia magaidi wa Daesh kueneza ugomvi wa kidini nchini humo.

Harakati ya kujitolea ya wananchi wa Iraq ina ushawishi mkubwa kati ya wananchi

 

Ali al Husaini amegusia pia matukio ya hivi karibuni nchini Iraq ya kukamatwa baadhi ya wanachama wa harakati hiyo na kusema, siku kadhaa zilizopita kumeanza vita vikubwa vya kipropaganda dhidi ya harakati hiyo ya wananchi wa Iraq kutoka kwa vyombo vya habari vya Magharibi na baadhi ya nchi za Kiarabu na lengo la propoaganda hizo ni kusahaulisha damu za wanamuqawama waliouawa shahidi nchini Iraq.

Wanajeshi magaidi wa Marekani, mapema Ijumaa asubuhi walivamia kituo cha brigedi za Hizbullah za Iraq katika eneo la al Daura mjini Baghdad wakiwa na magari 40 ya kijeshi na kutumia kikosi za kupambana na ugaidi cha Iraq na kuwateka nyara wanachama 13 wa brigedi hizo.

Hata hivyo msimamo imara ulioneshwa na makundi ya muqawama ya Iraq ulipelekea watu hao waachiliwe huru haraka sana.