Hamas yaitaka Mamlaka ya Ndani ya Palestina kuandaa kikao cha taifa
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i61912-hamas_yaitaka_mamlaka_ya_ndani_ya_palestina_kuandaa_kikao_cha_taifa
Mwakilishi wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amemtaka Mahmoud Abbas Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina kuandaa kikao cha taifa kwa ajili ya kubuni mkakati wa pamoja wa kukabiliana na mpango wa Israel wa kutaka kutwaa ardhi ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
(last modified 2026-02-25T03:34:48+00:00 )
Jun 30, 2020 03:23 UTC
  • Musa Abu Marzouq
    Musa Abu Marzouq

Mwakilishi wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amemtaka Mahmoud Abbas Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina kuandaa kikao cha taifa kwa ajili ya kubuni mkakati wa pamoja wa kukabiliana na mpango wa Israel wa kutaka kutwaa ardhi ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Musa Abu Marzouq amesema Hamas imewasiliana na nchi za Kiarabu na Kiislamu kwa shabaha ya kukabiliana na mpango wa kuyatwaa maeneo ya Ukingo wa Magharibi na kuyanganisha na ardhi zilizoghusubiwa za Palestina na inafanya juhudi za kuandaa mpango wa kitaifa wa kukabiliana na suala hilo.   

Abu Marzouq amesema, anataraji kuwa mpango wa kuyatwaa maeneo ya Ukingo wa Magharibi na kuyaunganisha na ardhi zilizoghusubiwa za Palestina utagonga mwamba kutokana na juhudi za makundi ya Palestina na nchi za Kiislamu na kwa kutumia nyenzo zote zilizopo kukabiliana na njama hiyo.  

Bonde la Mto Jordan ni miongoni mwa maeneo yaliyopangwa kutwaliwa na Israel 

Kwa mujibu wa mpango uliopendekezwa na Marekani wa "Muamala wa Karne", utawala wa Kizayuni wa Israel umepanga kuanza kutwaa maeneo ya Ukingo wa Magharibi na kuyaunganisha na ardhi za Palestina zilizoghusubiwa kuanzia mwezi ujao wa Julai. Eneo hilo linayojumuisha bonde la Jordan na vitongoji vyote vya walowezi wa Kizayuni katika Ukingo wa Magharibi mwa Mto Jordan.