Vyama mbalimbali Yemen vyapinga kuhuisha uhusiano na adui Mzayuni
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i62244-vyama_mbalimbali_yemen_vyapinga_kuhuisha_uhusiano_na_adui_mzayuni
Washiriki katika kikao kilichofanyika Sana'a mji mkuu wa Yemen wakiwakilisha vyama mbalimbali vya siasa na wawakilishi wa Palestina wamesisitiza udharura wa kusimama imara na bega kwa bega na wananchi wa Palestina na kupinga aina zote za kuanzishwa uhusiano na utawala ghasibu wa Israel.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 16, 2020 22:12 UTC
  • Vyama mbalimbali Yemen vyapinga kuhuisha uhusiano na adui Mzayuni

Washiriki katika kikao kilichofanyika Sana'a mji mkuu wa Yemen wakiwakilisha vyama mbalimbali vya siasa na wawakilishi wa Palestina wamesisitiza udharura wa kusimama imara na bega kwa bega na wananchi wa Palestina na kupinga aina zote za kuanzishwa uhusiano na utawala ghasibu wa Israel.

Televisheni ya al Masira ya Yemen imeripoti kuwa, vyama vya siasa vya Yemen na wawakilishi wa harakati za mapambano ya ukombozi za Palestina jana Alhamisi walifanya kikao mjini Sana'a na kusisitiza kuwa kuanzisha uhusiano na adui Mzayuni ni haramu na kinyume cha mafundisho ya dini. 

Wawakilishi wa vyama vya kisiasa vya Yemen na wa makundi ya Palestina katika kikao mjini Sana'a Yemen  

Hassan Hamran Mkuu wa faili la Palestina katika harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema Wayemeni wataendelea kuwa bega kwa bega na wananchi madhlumu wa Palestina hadi ardhi yote ya Palestina itakapokombolewa.

Naye Moaz Abu Shammalah, mwakilishi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) nchini Yemen ameeleza kuwa mpango habithi uliopewa jina la " Muamala wa Karne" ni awamu ya mwisho ya njama ya Marekani ya kusambaratisha malengo ya Palestina.  

Wakati huo huo Yahya Abu Usbu ambaye ni mwakilishi wa chama cha Kisoshalisti cha huko Yemen ameeleza kuwa, inasikitisha sana kuona pesa za nchi za Kiarabu zinatumika kutekeleza njama dhidi ya taifa la Palestina na kufungia mikataba ya kufedhehesha ili kuangamiza kadhia ya Palestina.