Ansarullah: Kambi ya Muqawama itaendelea kukabiliana na Marekani, Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i62451-ansarullah_kambi_ya_muqawama_itaendelea_kukabiliana_na_marekani_israel
Harakati ya Ansarullah ya wananchi wa Yemen imetangaza kuwa pande zote za Muqawama ni kambi moja inayopambana na ubeberu wa Marekani.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jul 27, 2020 12:17 UTC
  • Mohamed al-Bukhaiti
    Mohamed al-Bukhaiti

Harakati ya Ansarullah ya wananchi wa Yemen imetangaza kuwa pande zote za Muqawama ni kambi moja inayopambana na ubeberu wa Marekani.

Mohamed al-Bukhaiti ambaye ni mjumbe wa Idara ya Siasa ya harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema kuwa, harakati hiyo na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni kambi moja katika vita vya pande zote dhidi ya Marekani na Israel. 

Kuhusu hatua ya ndege za kivita za Marekani ya kutatiza safari ya ndege ya abiria ya Iran katika anga ya Syria na kutishia uhai wa abiria wake, Al-Bukhaiti amesema kuwa, Ansurullah itaainisha aina ya jibu la hatua hiyo ya Marekani kaika wakati mwafaka. Hata hivyo amesisitiza kuwa, jibu la Ansarullah si mbadala wa jibu litakalotolewa na Jamhuri ya kiislamu ya Iran kwa kitendo hicho cha ndege za kivita za Marekani. 

Mohamed al-Bukhaiti amesisitiza kuwa taifa la Yemen litaendelea kusimama bega kwa bega ya wapigania uhuru na haki kote duniani kwa ajili ya kupambana na ubabe na chokochoko za Marekani. 

Usiku wa kuamkia Alkhamisi iliyopita ndege mbili za kivita za Marekani zilitatiza safari ya ndege ya abiria ya Iran iliyokuwa katika anga ya Syria ikielekea Beirut. Baada ya hatua hiyo hatari na ya kihasama ya ndege hizo mbili za kivita, rubani wa ndege ya abiria ya Shrika la Ndege la Mahan la Iran alipunguza kasi ya mwendo wa chombo hicho kwa ghafla, suala ambalo limesababisha majeruhi kwa baadhi ya abiria. 

Watoto majeruhi walikowemo katika ndege ya abiria ya Iran

Baada ya tukio hilo la kihasama, mwakilishi wa Iran katika Umoja wa Mataifa, Majid Takht-Ravanchi amewasiliana na Katibu Mkuu wa Umoja huo, Antonio Guterres na kusisitiza kuwa, Marekani itabebeshwa dhima na lawama za tukio lolote litakalotokea wakati ndege hiyo itakapokuwa njiani kurejea nchini.