Hamas yapinga vikali kutiwa mbaroni Sheikh Raed Salah
(last modified Mon, 17 Aug 2020 02:29:47 GMT )
Aug 17, 2020 02:29 UTC
  • Hamas yapinga vikali kutiwa mbaroni Sheikh Raed Salah

Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesema kuwa hatua ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kumtia tena mbaroni kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Palestina ina lengo la kuwafutilia mbali walinzi wa Msikiti wa Al Aqsa.

Hazim Qassim amesema kuwa mienedo ya kutumia mabavu ya Wazayuni dhidi ya Msikiti wa Al Aqsa na walinzi wa msikiti huo inadhiihrisha namna utawala wa Kizayuni unavyopuuza hisia za Waislamu duniani. 

Hazim Qassim, Msemaji wa Hamas 

Sheikh Raed Salah ambaye ni kiongozi wa Harakati ya Kiislamu katika ardhi ya Palestina iliyokaliwa kwa mabavu mwaka 1948 tangu jana asubuhi alipelekwa katika jela iliyo karibu na mji wa Haifa ili kutumikia kifungo chake. 

Mahakama ya utawala wa Kizayuni wa Israel imemhukumu kifungo cha miezi 28 jela kiongozi huyo wa Harakati ya Kiislamu ya Palestina kwa tuhuma eti za kuchochea ghasia na kuongoza harakati hiyo ya Kiislamu. 

Tags