OIC yalaani jinai za Israel kaskazini mwa Ukanda wa Gaza
(last modified 2024-10-16T04:27:23+00:00 )
Oct 16, 2024 04:27 UTC
  • OIC yalaani jinai za Israel kaskazini mwa Ukanda wa Gaza

Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imelaani vikali mwenendo wa kushadidi jinai za kivita za utawala haramu wa Israel dhidi ya Wapalestina hususan katika maeneo ya kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.

Taarifa ya OIC sambamba na kulaani jinai za Israel imeeleza kuwa, hatua hizo za kinyama zinafanyika ili kuwahamisha kwa lazima Wapalestina, kufanya maangamizi ya kizazi na mauaji ya kimbari dhidi ya taifa la Palestina.

Sehemu nyingine ya taarifa ya Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imesema, Israel inabeba dhima ya kuuendelea vita na ugaidi wa kimataifa dhidi ya wananchi wa Palestina.

OIC imetaka kuchukuliwa hatua za kuwekea vikwazo utawala ghasibu wa Israel, kushtakiwa viongozi wake kwa kuhusika na mauaji na jinai dhidi ya binadamu na umelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

 

Wakati huo huo, Umoja wa Mataifa umesisitizia wito wa kusitishwa kwa mapigano nchini Lebanon na katika Ukanda wa Gaza kama njia moja ya kuzuia kutokea kwa mzozo zaidi mashariki ya kati, hatua ambayo UN inasema itaathiri dunia nzima.

Wito wake umekuja wakati huu utawala wa Kizayuni wa Israel ikiripotiwa kuendelea kutekeleza mashambulio inayosema yanawalenga wapiganaji wa Hezbollah.

Wakati hayo yakijiri jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel limeishambulia kwa mabomu kambi ya wakimbizi katika eneo la kati la Ukanda wa Gaza na kusababisha moto mkubwa uliopelekea kuuawa shahidi Wapalestina waliokuwa wametafuta hifadhi kwenye eneo hilo kutokana na hilaki ya vita vya mauaji ya kimbari vinavyoendelezwa na utawala huo ghasibu.

Tags