Moscow: Magaidi wa Jabhatu Nusra wanapanga kufanya mashambulizi ya kemikali Syria
Wizara ya Ulinzi ya Russia imetahadharisha kuwa, kundi la kigaidi la Jabhatu Nusra linajitayarisha kufanya mashambulizi ya silaha za kemikali katika mkoa wa Idlib nchini Syria.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Syria (SANA), mkuu wa kitengo cha uratibu cha Russia Aleksander Garkovic amesema kuwa, ripoti za upelelezi zinaonesha kuwa, magaidi wa kundi la Jabhatu Nusra wanajitayarisha kufanya mashambulizi ya silaha za kemikali kusini mwa eneo linalojulikana kama ukanda wa kupunguza mivutano katika mkoa wa Idlib.
Afisa huyo wa Russia amesema kuwa, magaidi hao wamejipanga kufanya hujuma hiyo ya kichochezi katika eneo la Jabal al Zawiya wakiwashirikisha baadhi ya waandishi wa habari wa kigeni ili baadaye picha hizo zitumiwe kulisingizia jeshi la taifa la Syria katika matangazo ya vyombo vya habari.
Habari za uongo kwamba serikali ya Syria inatumia silaha za kemikali dhidi ya makundi ya waasi daima zimekuwa zikitumiwa kama kisingizio cha mashambulizi ya kijeshi ya Marekani na waitifaki wake dhidi ya ardhi nchi hiyo na kushambulia miundombinu ya Syria hususan taasisi za kijeshi na kiuchumi.
Marekani inafanya mashambulizi hayo kuyalinda ili makundi ya kigaidi yanayoelekea kuangamizwa kikamilifu nchini Syria.