Muungano vamizi unaoongozwa na Saudia watekeleza njama mpya kusini mwa Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i65882-muungano_vamizi_unaoongozwa_na_saudia_watekeleza_njama_mpya_kusini_mwa_yemen
Kitengo cha Upashaji Habarii katika mikoa ya kusini mwa Yemen kimeripoti kuwa muungano vamizi huko Yemen unaoongozwa na Saudi Arabia unatekeleza njama mpya ili kuasisi vituo vya magaidi wa kitakfiri na ujasusi wa kisasa katika maeneo ya mikoa hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 19, 2021 23:15 UTC
  • Muungano vamizi unaoongozwa na Saudia watekeleza njama mpya kusini mwa Yemen

Kitengo cha Upashaji Habarii katika mikoa ya kusini mwa Yemen kimeripoti kuwa muungano vamizi huko Yemen unaoongozwa na Saudi Arabia unatekeleza njama mpya ili kuasisi vituo vya magaidi wa kitakfiri na ujasusi wa kisasa katika maeneo ya mikoa hiyo.

Kitengo cha Upashaji Habari katika mikoa ya kusini mwa Yemen kimeripoti kuwa, nchi wanachama katika muungano vamizi huko Yemen chini ya uongozi wa Saudi Arabia hivi karibuni zimeasisi zaidi ya vituo vipya  13 vya matakfiri katika mikoa ya Lahij, al Mohra, al Dhali'i na Shabwah; ambavyo lengo la kuasisiwa kwake ni kuyafadhili kifedha makundi ya kigaidi na yale yenye kufurutu ada.  

Kitengo hicho cha Upashaji Habari katika mikoa ya kusini mwa Yemen kimeongeza kuwa, nchi wanachama wa muungano vamizi huko Yemen unaoongozwa na Saudi Arabia zimeasisi kituo kimoja cha Kiwahabi katika eneo la Tur al Bahah na kingine cha Kisalafi katika mkoa wa Lahij. Nchi hizo wanachama wa muungano vamizi huko Yemen aidha zina mpango wa kuasisi vituo vingine sita vya Kiwahabi katika maeneo mengine ya Taiz huko Lahij.  

Njama mpya za muungano vamizi wa Saudia kusini mwa Yemen 

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, nchi hizo washirika katika muungano vamizi huko Yemen unaoongozwa na Saudia pia zinavifadhili kifedha vituo vingine vidogo 20 ili kueneza mafundisho na fikra za kigaidi na kitakfiri miongoni mwa vijana. 

Kitengo hicho cha Upashaji Habari katika mikoa ya kusini mwa Yemen  kimesisitiza kuwa, kuasisiwa vituo hivyo kunadhihirisha njama zilizoratibiwa na Israel na Marekani na kutekelezwa na Saudi Arabia na Imarati kwa ajili ya kuvuruga amani na uthabiti wa wananchi wa Yemen.