Makao ya uongozi mpya wa Daesh huko al Anbar yasambaratishwa
(last modified Fri, 29 Jan 2021 02:06:09 GMT )
Jan 29, 2021 02:06 UTC
  • Makao ya uongozi mpya wa Daesh  huko al Anbar yasambaratishwa

Wapiganaji wa Harakati ya Hashdu Shaabi ya Iraq wamesambaratisha makao ya uongozi wa kundi la kigaidi la Daesh katika eneo la jangwani katika mkoa wa al Anbar magharibi mwa nchi hiyo.

Qassim Mosleh Kamanda wa oparesheni wa Hashdu Shaabi katika mkoa wa al Anbar ametangaza taarifa ya kusabaratishwa makao  ya kundi la kigaidi la Daesh mkoani humo. 

Mosleh ameeleza kuwa oparesheni ya usalama iliyoanza katika upande wa magharibi mwa mkoa wa al Anbar kwa uratibu wa kikosi cha pamoja cha oparesheni, ndege za kivita za jeshi la Iraq na kikosi cha Hashdu Shaabi kulingana na taarifa sahihi walizopata imekuwa na mafanikio. 

Wapiganaji wa Hashdu Shaabi wa Iraq

Ameongeza kuwa, katika oparesheni hiyo makao ya uongozi mpya wa Daesh katika jangwa la magharibi mwa al Anbar katike eneo la Wadi al Mulsa  pamoja na makao nyingine saba zilizoasisiwa na kundi hilo la kigaidi zimesambaratishwa. 

Kamanda wa Hashdu Shaabi aidha ameeleza kuwa, magaidi wa Daesh walikuwa na lengo la kutekeleza oparesheni kisirisiri kwa kuvalia sare za askari usalama hata hivyo mpango wao huo pia umegonga mwamba.