Sheikh Naeem Qassim: Mazungumzo na Marekani hayana maana
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i66520-sheikh_naeem_qassim_mazungumzo_na_marekani_hayana_maana
Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema mazungumzo na serikali ya Marekani hayana maana.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 06, 2021 01:21 UTC
  • Sheikh Naeem Qassim: Mazungumzo na Marekani hayana maana

Naibu Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema mazungumzo na serikali ya Marekani hayana maana.

Sheikh Naeem Qassim, Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah ameyasema hayo Ijumaa katika mahojiano na Radio Noor ambapo amesema Hizbullah inakerwa na jambo moja tu muhimu nalo ni uwepo wa Wazayuni maghasibu katika eneo. Ameongeza kuwa, katika mazungumzo yoyote tayarajiwa na Marekani na Wazayuni, serikali ya Marekani itauunga mkono utawala wa Kizayuni wa Israel ambao unakalia ardhi za wengine kwa mabavu.

Sheikh Naeem Qassim ameongeza kuwa, Wazayuni daima wako katika hali ya kuhujumu lakini mhimili wa muqawama unalenga kulinda mamlaka ya kujitawala na uhuru wa Lebanon. Ameongeza kuwa Hizbullah inazuia utawala wa Kizayuni wa Israel kuivamia Lebanon.

Mpaka wa Lebanon na  ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel)

Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah aidha amesisitiza kuhusu kuundwa serikali mpya nchini Lebanon na kuongeza kuwa, watu wa Lebanon wanataka serikali iundwe haraka iwezekanavyo na hivyo wote wanapaswa kujitajidi kuhakikisha kuwa serikali shirikishi inaundwa.