Mbunge: Marekani inaunga mkono magaidi katika nchi za Syria na Iraq
Mbunge mmoja wa Syria amesema kuwa serikali ya Marekani inahusika katika ongezeko la hujuma za kigaidi nchini Syria na Iraq.
Ali al-Ali al-Abdo Al-Sattouf mjumbe katika Bunge la Syria ameliambia Shirika la Habari la Al-Ma'loumah kuwa kile ambacho kinajiri katika maeneo ya Al-Jazeera, Al-Hasakah, Al-Qashmili nchini Syria na pia katika baadhi ya maeneo ya jangwani nchini humo ni njama za Marekani zenye lengo la kuwarejesha magaidi wa ISIS au Daesh katika eneo hilo. Aidha amebainisha kuwa, lengo la Marekani katika kuwaunga mkono magaidi wa ISIS ni kuzigawa vipande vipande nchi za eneo hili.
Ameongeza kuwa serikali mpya ya Joe Biden nchini Marekani inaunga mkono magaidi ambao wamezingira maeneo ya al-Hasakah na Qashmali. Mbunge huyo wa Syria amesisitiza kuwa, njia pekee ya kukabiliana na uwepo wa majeshi wa Marekani katika eneo hili ni muqawama na mapambano.
Hivi sasa baadhi ya maeneo ya Syria na Iraq yameshuhudia ongezeko la hujuma za kigaidi zinazofanywa na magaidi wa ISIS waliosalia na ambao wamejificha miongoni mwa raia.
Hivi karibuni duru mbalimbali za habari ziliarifu kuwa, silaha na zana za kilojistiki za wanajaeshi magaidi wa Marekani zimeonekana zikiingizwa katika maidani ya mafuta huko Koniko kaskazini mashariki mwa Deir Zor.
Shirika la habari la Syria, SANA wiki iliyopita liliripoti kuwa msafara wa wanajeshi wa Marekani uliwasili katika maidani ya mafuta vya Koniko kaskazini mashariki mwa mkoa wa Deir Zor. Msafara huo wa wanajeshi wa Marekani ulikuwa umejizatiti kwa silaha na zana za kilojistiki.
Katika siku na miezi ya karibuni wanajeshi wa Marekani waliingiza mamia ya magari wao katika mkoa wa al-Hasakah kupitia vivuko haramu ili kutumika katika kambi zake za kijeshi na kuyasaidia pia makundi ya kigaidi na taasisi zake vibaraka.