Israel imebomoa majengo 178 ya Wapalestina mwaka huu wa 2021
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i66846-israel_imebomoa_majengo_178_ya_wapalestina_mwaka_huu_wa_2021
Jeshi la utawala haramu wa Israel limebomoa majengo 178 ya Wapalestina katika eneo unalolikalia kwa mabavu la Ukingo wa Magharibi katika mwaka huu wa 2021.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 14, 2021 09:14 UTC
  • Israel imebomoa majengo 178 ya Wapalestina mwaka huu wa 2021

Jeshi la utawala haramu wa Israel limebomoa majengo 178 ya Wapalestina katika eneo unalolikalia kwa mabavu la Ukingo wa Magharibi katika mwaka huu wa 2021.

Kwa mujibu wa taarifa, katika bomoa bomoa hiyo Wapalestina 259 wameachwa bila makazo wakiwemo watoto 140.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Palestina ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuratibu Misaada ya Kibinadamu (OCHA), bomoa bomoa ya hivi karibuni imejiri katika jijiji cha Humsa cha  jamii ya Wabedoui katika Bonde la Jordan.

Wakuu wa utawala dhalimu wa Israel wanaendeleza jinai hiyo ya kubomoa nyumba za Wapalestina mashariki mwa Quds (Jerusalem) na Eneo C katika Ukingo wa Magharibi.

Weledi wa mambo wanasema utawala wa Israel unabomoa nyumba hizo ili kuwaacha Wapalestina bila chaguo jingine ila kuondoka katika ardhi zao za jadi na kuwa wakimbizi.

Mji wa Quds

Mwaka 2020, wanajeshi wa Israel walibomoa nyumba 900 za Wapalestina na kuwaacha maelefu bila makazi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Utawala wa kikoloni wa Israel unakalia kwa mabavu ardhi za Palestina na unawanyima Wapalestina haki ya kutumia ardhi zao watakavyo. Wakati huo huo utawala huo dhalimu unaendeleza ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayauni katika ardhi unazozipora za Wapalestina katika maeneo ya Ukingo wa Magharibi.

Kwa mujibu wa sheria za kimataifa maeneo ya magharibi na mashariki mwa Quds yanatambuliwa kuwa ardhi ambazo zimekaliwa kwa mabavu na hivyo hatua zozote za ujenzi ambazo zinatekelezwa na utawala wa Kizayuni ni kinyume cha sheria.