Msafara wa wanajeshi vamizi wa Marekani washambuliwa kusini mwa Iraq
(last modified Wed, 14 Apr 2021 02:36:06 GMT )
Apr 14, 2021 02:36 UTC
  • Msafara wa wanajeshi vamizi wa Marekani washambuliwa kusini mwa Iraq

Duru za habari za Iraq zimetangaza kuwa, msafara wa magari yaliyokuwa yamepakia vifaa mbalimbali na zana za kijeshi kwa ajili ya wanajeshi vamizi wa Marekani umeshambuliwa kusini mwa nchi hiyo.

Tovuti ya habari ya Saberin News imeripoti kuwa, msafara uliokuwa na misaada kwa ajili ya jeshi la Marekani umeshambuliwa katika mji wa Samawah katika mkoa wa Al Muthanna kusini mwa Iraq.

Duru za Iraq hadi sasa hazijatoa maelezo zaidi kuhusu idadi ya watu waliouawa na hasara nyingine zilizosababishwa na shambulio hilo. Aidha hakuna kundi lolote hadi sasa lililotangaza kuhusika na shambulio hilo dhidi ya msafara wa wanajeshi wa Marekani huko Iraq. 

Wanajeshi vamizi wa Marekani nchini Iraq   

Mashambulizi mengi sawa na hili lililoripotiwa kutekelezwa dhidi ya msafara wa jeshi la Marekani huko al Muthanna kusini mwa Iraq yamejiri katika miezi ya hivi karibuni dhidi ya vikosi vamizi vya Marekani.  

Shambulio hilo limejiri huku Bunge la Iraq likiwa tayari limepasisha mpango wa kuwafukuza nchini humo wanajeshi wa nchi ajinabi. Wananchi na mukundi ya Kiiraqi pia yanataka kuondoka wanajeshi wa Marekani nchini humo.