Serikali ya Saudia yabomoa msikiti mwingine wa Waislamu wa Kishia
(last modified Sat, 24 Apr 2021 12:38:18 GMT )
Apr 24, 2021 12:38 UTC
  • Serikali ya Saudia yabomoa msikiti mwingine wa Waislamu wa Kishia

Mabuldoza ya utawala wa Aal Saud yamebomoa msikiti mwingine ulioko kandokando ya mji wa Qatif ambao wakazi wake ni Waislamu wa madhehebu ya Shia mashariki ya Saudi Arabia.

Wanaharakati wa mitandao ya kijamii nchini Saudi Arabia wameripoti kuwa tukio hilo la kubomolewa msikiti huo ulioko katika kijiji cha Ummul-Hamaam kwenye kiunga cha mji wa Qatif mashariki ya nchi hiyo limejiri wakati wa usiku.

Kwa mujbu wa ripoti hizo, mabulodoza ya utawala wa Aal Saud yamechukua hatua ya kuubomoa kikamilifu msikiti huo kwa kisingizio cha kutaka kupanua barabara.

Huo ni msikiti wa pili kuvunjwa na serikali ya Riyadh katika kipindi cha miezi mitano iliyopita katika eneo la Ash-Sharqiyyah nchini Saudi Arabia.

Shahid Sheikh Nimr Baqir An-Nimr 

Mnamo mwezi Desemba 2020 pia utawala wa Aal Saud uliubomoa na kuusawazisha kikamilifu na ardhi msikiti wa Imam Hussein (as) katika mji wa al-A'waamiyyah, msikiti ambao Shahid Sheikh Nimr Baqir An-Nimr alikuwa akisalisha na kutoa hotuba na mihadhara ndani yake.../