Sep 05, 2024 06:03 UTC
  • Mvua na mafuriko yabomoa Msikiti mkongwe zaidi Niger

Maafa ya mvua na mafuriko yanaendelea kushuhudiwa katika maeneo mbalimbali za magharibi mwa Afrika na kusababisha maafa makubwa ikiwa ni pamoja na kubomoa Msikiti mkongwe zaidi nchini Niger.

Msikiti wa Zinder, ambao ni mmoja wa Misikiti mikongwe zaidi nchini Niger, umebomoka kutokana na mvua hizo za masika.

Afŕika Maghaŕibi hupata mvua nyingi na ardhi yake kuwa nyevunyevu sana wakati wa msimu wa mvua ambao huanzia mwezi Juni na kuendelea hadi mwezi Septemba kila mwaka.

Msikiti wa Zinder ambao ni nembo ya kihistoria kwa Niger na Ulimwengu wa Kiislamu, umebomoka kutokana na mvua kubwa inayoendelea kunyesha.

Msikiti huo ulijengwa takriban mwaka 1852 na Sultan Tanimoune Dan Souleymane. Umo katika orodha ya misikiti iliyotembelewa zaidi nchini humo, baada ya ule wa Agadez uliojengwa mwaka 1515 Milaadia.

Eneo la Zinder, lililoko kusini-mashariki mwa Niger, ni moja ya maeneo yaliyoathiriwa zaidi na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini humo tangu mwezi Juni.

Tags