Frangieh: Marekani haina uwezo wa kuidhoofisha Hizbullah
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i7936-frangieh_marekani_haina_uwezo_wa_kuidhoofisha_hizbullah
Mkuu wa harakati ya el Marada ya Lebanon amesema kuwa, vikwazo vya kifedha vilivyowekwa na Marekani dhidi ya Hizbullah haviwezi kuidhoofisha harakati hiyo ya muqawama wa Kiislamu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 27, 2016 23:17 UTC
  • Frangieh: Marekani haina uwezo wa kuidhoofisha Hizbullah

Mkuu wa harakati ya el Marada ya Lebanon amesema kuwa, vikwazo vya kifedha vilivyowekwa na Marekani dhidi ya Hizbullah haviwezi kuidhoofisha harakati hiyo ya muqawama wa Kiislamu.

Shirika la habari la IRNA limemnukuu Suleiman Frangieh akisema hayo jana (Ijumaa) na kuongeza kuwa, njama za Washington la kuzishinikiza benki na serikali ya Lebanon ili zikubali kushirinikiana nayo katika vikwazo hivyo hazitosaidia kitu. Amesisitiza kuwa, uzoefu unaonesha kwamba vikwazo huwa na matokeo tofauti na yanayotarajiwa na maadui na kwamba vikwazo vya hivi sasa vya Marekani dhidi ya Hizbullah vitazidisha tu ushawishi na nguvu za harakati hiyo na kuifanya kuwa na misimamo imara zaidi. Suleiman Frangieh ameinahisi kwa njia isiyo ya moja kwa moja Marekani akiitaka ipate funzo kutoka katika historia ya huko nyuma na itarajie kupata matokeo tofauti kabisa na inayoyatarajia. Baada ya kupasisha vikwazo vya kifedha dhidi ya Hizbullah kwa ajili ya kudhamini manufaa ya utawala wa Kizayuni wa Israel na Saudia, serikali ya Maerekani imemtuma Waziri wake wa Hazina mjini Beirut ili kuishinikiza serikali ya Lebanon ikubali kushirikiana nayo katika vikwazo dhidi ya Hizbullah. Hata hivyo Suleiman Frangieh, mkuu wa harakati ya el Marada ya Lebanon ameashiria katika maneno yake kuwa, inaonekana Wamarekani hawajui nafasi ya Hizbullah nchini Lebanon na kusema kuwa, Washington haina uwezo wa kuidhoofisha harakati hiyo ya muqawama wa Kiislamu.