Kamanda mwandamizi wa Imarati auawa mjini Aden, Yemen
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i81752-kamanda_mwandamizi_wa_imarati_auawa_mjini_aden_yemen
Kamanda wa ngazi ya juu wa Umoja wa Falme za Kiarabu ameuawa katika mripuko wa bomu mjini Aden, kusini mwa Yemen.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Mar 25, 2022 02:29 UTC
  • Kamanda mwandamizi wa Imarati auawa mjini Aden, Yemen

Kamanda wa ngazi ya juu wa Umoja wa Falme za Kiarabu ameuawa katika mripuko wa bomu mjini Aden, kusini mwa Yemen.

Shirika la habari la Iran Press limenukuu shirika la Russia Today likisema kuwa, Brigedia Jenerali Sabet Muthanna Jawas ameuawa pamoja na mtoto wake wa kiume na watu wengine kadhaa aliokuwa ameandamana nao katika kijiji cha al-Madina al-Khadra, yapataka kilomita 10 kaskazini mwa mji bandari wa Aden.

Jenerali Jawas alikuwa mmoja wa makamanda waandamizi wanaoongoza mashambulizi ya vikosi vamizi vya muungano wa Saudia na Imarati dhidi ya harakati ya muqawama ya Ansarullah ya Yemen.

Anaripotiwa kuongoza operesheni iliyomuua shahidi kiongozi wa zamani wa harakati ya Ansarullah ya Yemen, Hussein Badreddin al-Houthi, katika mkoa wa Sa’ada mwaka 2004.

Askari vamizi wa Imarati nchini Yemen

Tangu Aprili 2020, wanamgambo wa Umoja wa Falme za Kiarabu wanaojiita Baraza la Mpito la Kusini (STC) walitangaza kuwa, watasimamia na kuendesha kivyao masuala ya mji wa bandari wa Aden na mikoa mingine ya kusini mwa nchi hiyo.

Hii ni katika hali ambayo, Muhammad al Aatifi, Waziri wa Ulinzi wa serikali ya uokovu wa kitaifa ya Yemen amesisitiza kuwa, muundo na sura ya muqawama katika siku zijazo utakuwa wa kutisha kwa nchi vamizi.