HAMAS: Vitisho vya Israel haviwezi kuwababaisha Wapalestina
Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amejibu matamshi ya kifedhuli ya Waziri wa Vita wa Israel, Benny Gantz na kusisitiza kuwa: Vitisho kamwe haviwezi kuwababaisha na kuwashtua Wapalestina
Hazem Qassem, Msemaji wa HAMAS katika radiamali yake kwa matamshi ya vitisho ya Gantz amesisitiza kuwa, "Matamshi kama hayo hayawezi kulishtua taifa la Palestina na kambi yake ya muqawama."
Aidha amesema matamshi ya Waziri wa Vita wa utawala haramu wa Israel hayawezi kuwafanya wananchi wa Palestina waachane na mapambano yao halali dhidi ya utawala huo ulioghusubu na kukalia kwa mabavu ardhi za Wapalestina.
Hazem Qassem, Msemaji wa HAMAS amebainisha kuwa: Mapinduzi haya yataendelea hadi pale watu wetu watakapofikia malengo makuu ya ukombozi na kurejea (katika ardhi zao za asili zilizoporwa).
Tangu mwezi mtukufu wa Ramadhani uanze, askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel wameshadidisha hujuma zao katika maeneo ya Palestina, jambo lililowasukuma pia wananchi wa Palestina na makundi ya muqawama yaanzishe operesheni za kujibu chochoko hizo.
Wazayuni kadhaa wameangamizwa katika operesheni hizo za kujitoa muhanga vijana na wanajihadi wa Kipalestina, hususan katika miji wa Tel Aviv na Jenin.