HAMAS: Marekani ni mshirika wa jinai za Israel dhidi ya Wapalestina
(last modified Thu, 18 Aug 2022 04:11:07 GMT )
Aug 18, 2022 04:11 UTC
  • HAMAS: Marekani ni mshirika wa jinai za Israel dhidi ya Wapalestina

Mousa Mohammed Abu Marzook, Naibu Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema kuwa, Marekani ni mshirika wa jinai zinazofanywa na utawala haramu wa Israel dhidi ya wananchi wa Palestina.

Mousa Abu Marzook amesema hayo katika radiamali yake kwa taarifa zilizosambaa zinazodai kuweko mawasiliano ya siri ya Marekani na harakati hiyo na kusisitiza kwamba, Marekani ni mshirika wa jinai za Israel dhidi ya wananchi wa Palestina na kwamba, licha ya Washington kuomba mara kadhaa kuweko mazungumzo rasmi baina yake na HAMAS lakini harakati hi imekataa.

Kiongozi huyo mwandamizi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS ameashiria njama mbalimbali na uungaji mkono wa Marekani kwa utawala haramu wa Israel unaotenda jinai kila uchao dhidi ya Wapalestina na kusisitiza kwamba, serikali ya Washington ni mshirika wa wazi kabisa wa jinai zinazofanywa na Israel dhidi wananchi madhulumu wa Palestina.

Mousa Mohammed Abu Marzook, Naibu Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS 

 

Marekani ni muungaji mkono mkuu wa jinai na ukatili wa utawala wa Kizayuni wa Israel na mara zote imekuwa ikitumia kura ya veto kukwamisha jaribio lolote la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la hata kuelezea wasiwasi wake tu kuhusu jinai za Israel.

Mbali na serikali zilizotangulia, hata serikali ya sasa ya Rais Joe Biden imetangaza mara kadhaa kuunga mkono jinai za Israel, huku utawala wa Kizayuni ukiendelea kufanya ukatili mkubwa kwa kushambulia kwa makombora na mabomu mazito makazi ya raia sambamba na kuendeleza ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika maeneo ya Wapalestina.

Tags