White House yakataa kuzungumza na Israel kuhusu JCPOA
(last modified Thu, 25 Aug 2022 12:07:06 GMT )
Aug 25, 2022 12:07 UTC
  • White House yakataa kuzungumza na Israel kuhusu JCPOA

Ikulu ya White House ya Marekani imeripotiwa kulipiga na chini ombi la Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel la kufanya mazungumzo ya simu 'ya dharura' na Rais Joe Biden, kuhusu mazungumzo yaliyko katika hatua za mwisho ya kujaribu kuhuisha makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.

Kanali ya 13 ya Kizayuni bila kutaja jina, imenukuu duru za Israel zikisema kuwa, Ofisi ya Rais wa Marekani imedai kuwa Biden yupo katika likizo ya wiki mbili na kwa msingi huo hawezi kufanya mazungumzo na Yair Lapid, Waziri Mkuu wa Israel.

Habari zaidi zinasema kuwa, Benny Gantz, Waziri wa Vita wa utawala haramu wa Israel hatakutana na Lloyd Austin, Waziri wa Ulinzi wa Marekani katika safari yake mjini Washington leo Alkhamisi.

Maafisa wa Tel Aviv hivi sasa wanatapatapa huku na kule, na kukerwa na ukweli kuwa yumkini mapatano ya kuiondolewa Iran vikwazo vya kidhalimu yatafikiwa karibuni hivi.

Kabla ya hapo, Waziri Mkuu katika serikali ya mseto ya Israel alionekana kuingiwa na kiwewe pia kutokana na uwezekano mkubwa wa kufikiwa makubaliano ya kuhuisha mapatano ya nyuklia ya JCPOA ndani ya siku chache zijazo.

Mazungumzo ya Vienna

Katika ujumbe wa Twitter, Naftali Bennett amesema, "Natoa mwito kwa Rais wa Marekani Joe Biden, na utawala wa Washington kujizuia, katika dakika hizi za mwisho, kusaini makubaliano na Iran." 

Anadai kuwa, kupasishwa kwa mapatano hayo kutaipa serikal ya Iran robo ya dola trilioni moja, fedha ambazo zitaiwezesha Tehran kuzalisha, kusimika na kuendesha mitambo ya mashinepewa pasi na kizuizi kwa miaka miwili.