Jan 31, 2023 02:23 UTC
  • Jumla ya Wapalestina 35 wameuliwa shahidi na Israel mwezi Januari pekee

Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza kuwa, mwezi Januari mwaka huu ndio mwezi uliojaa umwagaji damu mkubwa zaidi katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan baada ya utawala wa Kizayuni wa Israel kuwaua shahidi Wapalestina 38.

Wazayuni kila siku hushambulia maeneo mbalimbali ya Palestina ili kufanikisha malengo yao ya kujitanua; ambapo hadi sasa Wapalestina wengi wameuawa shahidi au kujeruhiwa na wanajeshi wa utawala haramu wa Israel.  

Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza kuwa, mwezi uliopita wa Januari ndio mwezi ulishuhudia umwagadi mkubwa wa damu katika eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan tangu mwaka 2015 hadi sasa, kufuatia kuuliwa shahidi Wapalestina 35 wakiwemo watoto 8. Raia hao wa Palestina wameuawa kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa utawala ghasibu wa Israel na walowezi wa Kiyahudi. 

Vijana wa Kipalestina, waliouliwa shahidi na Israel mwezi Januari 2023

Wizara ya Afya ya Palestina imeongeza kuwa, wanajeshi wa utawala wa Kizayuni waliwalenga na kuwashambulia Wapalestina wengi katika eneo hilo. Imeongeza kuwa, tangu kuanza mwaka huu wa 2023, Wapalestina 20 wameuliwa shahidi katika mji wa Jenin. Idadi hiyo ni kubwa kuwahi kusajiliwa huko Jenin. 

Ni zaidi ya miaka 70 sasa utawala ghasibu wa Israel unaendelea kutwaa na kughusubu haki za wananchi madhlumu wa Palestina. Katika miaka yote hiyo utawala haramu wa Israel umetenda jinai nyingi za kutisha na za kinyama dhidi ya Wapalestina. 

Tags