Ukandamizaji mkubwa wa wapinzani watanda maeneo tofauti ya 'Israel'
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i94686-ukandamizaji_mkubwa_wa_wapinzani_watanda_maeneo_tofauti_ya_'israel'
Wapinzani wa Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wamekandamizwa vikali na polisi wa Israel wakati wa maandamano yao makubwa ya leo Ijumaa.
(last modified 2026-07-11T07:59:36+00:00 )
Mar 03, 2023 06:40 UTC
  • Ukandamizaji mkubwa wa wapinzani watanda maeneo tofauti ya 'Israel'

Wapinzani wa Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wamekandamizwa vikali na polisi wa Israel wakati wa maandamano yao makubwa ya leo Ijumaa.

Hayo yameripotiwa na tovuti ya Shahab News ambayo pia imeweka picha za ukandamizaji mkubwa wa wapinzani uliofanywa na polisi wa Israel dhidi ya wapinzani wa Netanyahu. Wakati iliporipotiwa habari hii machafuko yalikuwa yanaendelea katika maeneo  tofauti ya ardhi ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni. Polisi walikuwa wamepiga kambi na wakikandamiza vikali maandamano hayo kwa kutumia zana mbalimbali yakiwemo mabomu ya kutoa machozi.

Vyombo vya habari vimeripoti habari hiyo kwa kusema: "Hii leo polisi wa Israel wamekabiliana vikali na waandamanaji wanaompinga Waziri Mkuu wa utawala huu, Netanyahu, wakisisitizia matakwa yao na kusema, kuwa wataendelea kukabiliana moja kwa moja na serikali ya Netanyahu."

Polisi wa utawala wa Kizayuni wakikandamiza wapinzani wa Netanyahu

Leo vyombo vya habari vya Kiebrania vimechapisha picha za maandamano makubwa ya wapinzani wa Netanyahu huko Tel Aviv, wakati waandamanaji walipovunja vizuizi vilivyowekwa na polisi wa Israeli na kushadidisha machafuko hayo. 

Ikumbukwe kuwa katika siku za hivi karibuni suala la mageuzi ya mahakama lililopendekezwa na Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni Benjamin Netanyahu limezusha malalamiko makubwa katika ardhi hizo zinazokaliwa kwa mabavu na Wazayuni.

Vyanzo vya habari vya Kiebrania vimeripoti kushiriki karibu waandamanaji 250,000 kwenye mitaa ya Tel Aviv, Baytul Muqaddas inayokaliwa kwa mabavu na miji mingine, jambo ambalo halijawahi kushuhudiwa katika maandamano ya huko nyuma ya kumpinga Netanyahu.