Ziyad al-Nakhalah: Wapalestina hawataruhusu mipango ya Wazayuni Palestina itekelezwe kivitendo
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i94728-ziyad_al_nakhalah_wapalestina_hawataruhusu_mipango_ya_wazayuni_palestina_itekelezwe_kivitendo
Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihadul-Islami ya Palestina amesema kuwa, wapiganaji shupavu wa Paalestina katu hawataruhusu mipango michafu ya Wazayuni huko Palestina itekelezwe kivitendo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 05, 2023 00:28 UTC
  • Ziyad al-Nakhalah:  Wapalestina hawataruhusu mipango ya Wazayuni Palestina itekelezwe kivitendo

Katibu Mkuu wa Harakati ya Jihadul-Islami ya Palestina amesema kuwa, wapiganaji shupavu wa Paalestina katu hawataruhusu mipango michafu ya Wazayuni huko Palestina itekelezwe kivitendo.

Ziyad al-Nakhalah amebainisha kwamba, mipango michafu ya Wazayuni dhidi ya mji mtakatifu wa Quds pamoja na njama zake za kuliyahudisha eneo hilo takatifu zitafeli na kugonga mwamba.

Kiongozi huyo wa Jihadul-Islami amesisitiza kwamba, wanamapambano wa Palestina wamejiandaa kikamilifu kukabiliana na njama za Wazayuni dhidi ya Baytul-Muqaddas na kwamba, hawataruhusu Wazayuni wafanikiwe kutekeleza kivitendo mipango yao michafui iliyojaa njama dhidi ya Wapalestina.

Amesema pia kuwa, Harakati ya Jihadul-Islami ya Palestina inasimama bega kwa bega na familia za Mashahidi na haitaacha kutekeleza jukumu lake la kudumu katika utiifu na uaminifu kwa Waplestina waliojitoa mhanga na kuendelea kuwafuata mashahidi hao hadi utakapotekelezwa usia wao wa kurejeshwa uhuru na haki kwa taifa la Palestina na Umma wa Kiislamu.

Vitongoji haramu vya walowezi wa Kizayuni

 

Hayo yanajiri katika hali ambayo, Jumatatu ya tarehe 20 Februari Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipasisha rasimu ya azimio linalolaani uamuzi wa serikali ya Israel yenye misimamo ya kufurutu ada ya Benjamin Netanyahu wa kuidhinisha ujenzi wa vitongoji vipya tisa katika ardhi za Wapalestina za Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Utawala huo ulizikaliwa kwa mabavu ardhi za Palestina katika vita vya mwaka 1967; na azimio la Geneva linasema kuwa ni marufuku utawala wa Kizayuni kufanya shughuli zozote za ujenzi katika ardhi hizo zinazokaliwa kwa mabavu.