-
Hamas: Witkoff aliahidi kuondoa mzingiro wa Gaza mkabala wa kuachiwa Edan Alexander
May 17, 2025 06:57Afisa mwandamizi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas amesema kuwa, mjumbe maalumu wa Marekani Steve Witkoff alilihakikishia kundi hilo la Muqawama la Palestina kwamba, Washington itaishinikiza Israel kukomesha mzingiro wa Gaza na kuruhusu ufikishaji wa misaada ya kibinadamu ndani ya siku mbili baada ya kumwachilia huru mwanajeshi wa Israel, Edan Alexander, raia wa Marekani.
-
Hofu ya kukamatwa yamfanya Netanyahu afute safari yake ya Vatican
May 17, 2025 04:00Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel amefuta safari yake ya Vatican akihofia kutekelezwa waranti wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC unaotaka atiwe mbaroni kwa kutenda jinai za kivita Palestina.
-
Umoja wa Mataifa: Uhaba wa chakula Gaza umefikia kiwango cha janga la njaa
May 17, 2025 03:58Ripoti ya Umoja wa Mataifa inaonyesha kuwa, uhaba mkubwa wa chakula katika Ukanda wa Gaza umefikia kiwango cha janga la njaa.
-
UNICEF: Israel imeua watoto 45 wauawa Gaza kwa muda wa siku mbili
May 17, 2025 03:57Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Kuhudumia Watoto (UNICEF) umetangaza kuwa, wanajeshi wa Israel wamewaua shahidi watoto 45 katika Ukanda wa Gaza ndani ya siku mbili.
-
Miaka 77 baada ya Siku ya Nakba; jinai zisizo na kikomo za Wazayuni na muqawama imara wa Wapalestina
May 16, 2025 07:33Ni miaka 77 imepita sasa tangu Siku ya Nakba. Jinai za Wazayuni zinazidi kushika kasi mno, na Wapalestina wanaendelea kusisitiza muqawama na kusimama kidete.
-
Ijumaa ya umwagaji damu Ghaza, mashahidi 250 katika masaa 36
May 16, 2025 06:55Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya ya Ghaza ametangaza leo Ijumaa kwamba ukanda huo ndilo eneo la mauaji ya umati ya kutisha zaidi katika siku za hivi karibuni kiasi kwamba Wapalestina 250 wameuliwa shahidi na Israel katika kipindi cha saa 36 zilizopita pekee.
-
Hamas yamjibu Trump: Ghaza si bidhaa ya kupigwa mnada
May 16, 2025 06:54Kiongozi mmoja wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS amejibu matamshi ya kijuba ya rais wa Marekani, Donald Trump alielezea nia ya Washington ya kuuteka Ukanda wa Ghaza na eti kuugeuza kuwa eneo huru, akimwambia, Ghaza si bidhaa ya kupigwa mnada.
-
Ansarullah: Iran imetekeleza wajibu wake wa Kiislamu kuiunga mkono Palestina
May 16, 2025 03:22Kiongozi wa Harakati ya Muqawama ya Ansarullah ya Yemen ameipongeza Iran kwa uungaji mkono wake usio na kikomo kwa taifa la Palestina na kadhia yao halali na kueleza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu inafuata njia ya heshima katika suala hilo na nchi nyingine zote za Kiislamu lazima zifuate mkondo huo.
-
Hamas: Maisha ya mateka wa Israel si muhimu kwa Netanyahu
May 15, 2025 22:51Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imetilia mkazo masharti yake makuu kuhusu makubaliano ya kudumu ya kusimamisha vita na kuondoka kikamilifu wanajeshi vamizi wa Israel kwenye Ukanda wa Ghaza ikitangaza kuwa, Netanyahu amefeli katika njama zake za kufikia makubaliano bila ya kusitisha vita kikamilifu na kwamba mateka wa Kizayuni si muhimu kwa Netanyahu.
-
Ukidhabi mkubwa wa Israel kuhusu mashambulizi yake dhidi ya hospitali za Ghaza wafichuka
May 15, 2025 22:50Gazeti moja la lugha ya Kiebrania limefichua kwamba jeshi la Israel lilitoa taarifa za uongo kuhusu kuwepo handaki la Hamas chini ya "Hospitali ya Ulaya" (The European Hospital) huko Khan Yunis, kusini mwa Ukanda wa Ghaza, na kwamba hospitali hiyo ililengwa na mashambulizi makubwa ya mabomu mara mbili ndani ya saa 24 bila ya kuweko handaki lolote la HAMAS.