-
Hizbullah: Adui Mzayuni hawezi kuusambaratisha muqawama
Feb 22, 2025 23:14Naibu Mkuu wa Baraza la Utendaji la Hizbullah ya Lebanon amesema: Adui Mzayuni hawezi kuusambaratisha muqawama.
-
IOM: Asilimia 90 ya nyumba za Gaza zimebomolewa
Feb 22, 2025 23:13Shirika la Kimataifa la Uhamiaji limetangaza kuwa, asilimia 90 ya nyumba katika Ukanda wa Gaza zimeharibiwa, na mamia ya maelfu ya Wapalestina hawana pa kwenda, na Wapalestina ambao wamerejea katika maeneo yao wanajikuta wakikabiliwa na vilima vya uchafu.
-
Kufichuka nia halisi ya utawala wa Kizayuni nchini Syria
Feb 22, 2025 23:11Kimya na kutochukua hatua yoyote watawala wapya wa Syria vimeufanya utawala wa Kizayuni wa Israel ufikirie kuyatwaa kabisa maeneo mapya yaliyokaliwa kwa mabavu nchini Syria.
-
HAMAS: Mateka 6 Waisrael wataachiwa leo mkabala wa Wapalestina 602 walioko kwenye jela za Israel
Feb 22, 2025 02:34Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imetangaza majina sita ya mateka Waisrael, ambao wanatazamiwa kuachiliwa leo katika mwendelezo wa awamu ya kwanza ya makubaliano ya kusitisha mapigano na kubadilishana mateka na utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Jeshi la Israel lawaua kwa kuwapiga risasi watoto wa miaka 12 na 13 Wapalestina Ukingo wa Magharibi
Feb 22, 2025 02:34Watoto wawili wa Kipalestina wenye umri wa miaka 12 na 13 wameuawa shahidi kwa kupigwa risasi na askari wa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel wakati wa mfululizo wa mashambulizi mengi yaliyofanywa na jeshi hilo usiku kucha wa kuamkia leo katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu yakijumuisha maeneo ya Tulkarem, Jenin na Nablus.
-
Israel yampiga marufuku msomi maarufu wa Kiislamu kuingia Msikiti wa Al-Aqsa
Feb 21, 2025 23:41Vikosi vya utawala vamizi wa Israel vimemkamata na kumpiga marufuku Sheikh Najeh Bakirat, kiongozi mashuhuri wa Kiislamu Palestina kuingia katika Msikiti wa Al-Aqsa ulioko jijini Al Quds (Jerusalem).
-
UN: Inahitajika zaidi ya nusu karne kuufufua uchumi wa Syria urejee kwenye hali ya kabla ya vita
Feb 21, 2025 23:32Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa Syria inahitaji muda wa zaidi ya nusu karne ili kurejea kwenye hali yake ya uchumi ya kabla ya vita angamizi vya ndani ya nchi hiyo.
-
Mateka wa Kizayuni: Kwa muda wote walipotushikilia, Al-Qassam waliamiliana nasi kwa wema
Feb 21, 2025 07:27Gazeti moja la Kizayuni limemnukuu mateka mmoja Muisrael akisema kuwa Wanamuqawama wa Brigedi za al-Qassam, tawi la kijeshi la harakati ya HAMAS waliamiliana kwa wema na mateka hao wa Kizayuni kwa muda wote walipokuwa wakiwashikilia huko Ukanda wa Ghaza.
-
Netanyahu adai mabaki ya mwili yaliyorejeshwa si ya Shiri Bibas, HAMAS yamjibu
Feb 21, 2025 07:24Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel amedai kuwa harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS imekiuka masharti ya makubaliano ya kubadilishana mateka kwa sababu imekabidhi mwili wa mwanamke asiyejulikana kutoka Ghaza badala ya ule wa mateka wa Kizayuni Shiri Bibas.
-
Askofu Mkuu wa Quds: Palestina, kamwe haitomsahau Nasrullah
Feb 21, 2025 03:21Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiorthodoksi la Ugiriki katika mji mtukufu wa al-Quds unaokaliwa kwa mabavu, Atallah Hanna, amemuenzi na kumsifu aliyekuwa Kiongozi wa Harakati ya Muqawama ya Hizbullah nchini Lebanon, Sayyid Hassan Nasralluh, akisisitiza kuwa watu wa Palestina daima wataendelea kuwa waaminifu kwake kwa namna alivyojitolea muhanga.