Hizbullah: Adui Mzayuni hawezi kuusambaratisha muqawama
Naibu Mkuu wa Baraza la Utendaji la Hizbullah ya Lebanon amesema: Adui Mzayuni hawezi kuusambaratisha muqawama.
Shheikh Ali Da'mush amesema hayo wakati wa mkutano na waandishi wa habari wa kamati kuu ya shughuli ya mazishi ya Seyed Hassan Nasrullah na Seyed Hashem Safieddin ambapo sambamba na kutoa heshima zake kwa familia za mashahidi hawa wawili waheshimiwa amesema, kuuawa shahidi shakhsia hawa wakubwa halikuwa jambo la kushtukiza kwetu kwa sababu sisi ni watu wa shule ambayo maimamu, viongozi na wanachuoni wote wameuawa shahidi.
Kiongozi huyo wa ngazi ya juuu wa Hizbullah amesema, bendera ya Hizbullah kamwe haitaanguka chini, kama tulivyosimama katika hatua zote za muuqawama dhidi ya adui Mzayuni.
Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA, miili ya Mashahidi Sayyid Hassan Nasrullah, Katibu Mkuu wa zamani wa Hizbullah ya Lebanon, na naibu wake Sayyid Hashim Safiyyuddin, imepangwa kuzikwa kusini mwa Lebanon leo Jumapili Februari 23, 2025.
Shahidi Sayyid Hassan Nasrullah, ambaye alihudumu kama Katibu Mkuu wa Hizbullah kwa zaidi ya miaka 30, aliuawa shahidi siku ya Ijumaa ya tarehe 27 Septemba katika shambulio la kigaidi la anga lililofanywa na jeshi la utawala wa Kizayuni katika eneo la viunga vya kusini mwa Beirut.
Naye Shahidi Hashem Safiyyuddin, Mkuu wa Baraza la Kisiasa la harakati hiyo ya Muqawama aliuawa shahidi katika shambulio jengine la kigaidi lililofanywa na Israel karibu wiki moja baada ya kuuawa shahidi Sayyid Hassan Nasrullah.