-
Kiongozi wa Kataib Hizbullah ya Iraq aapa kuendeleza njia ya mapambano, apinga vitisho vya adui
Jul 12, 2026 04:17Katibu Mkuu wa Kataib Hizbullah nchini Iraq amesema kundi lake litaendeleza njia ya Muqawama na mapambano, akipuuza vitisho vya maadui na kuwataka maafisa wa serikali ya nchi hiyo na viongozi wa kisiasa kuheshimu matakwa ya taifa hilo la Kiarabu.
-
Matamshi ya Waziri wa Vita wa Israel kuhusu Lebanon yana taathira gani?
Jul 11, 2026 07:49Israel Katz, Waziri wa Vita wa utawala ghasibu wa Israel, amejibu matamshi ya hivi karibuni ya Donald Trump kuhusu kuondoka Israel katika ardhi ya Lebanon kwa kuyapinga vikali, na kusema Israel haitaomba idhini ya mtu yoyote katika kuendelea kusalia nchini Lebanon.
-
Familia nzima imeangamizwa: Amnesty International yaituhumu Israel kufanya uhalifu wa kivita nchini Lebanon
Jul 11, 2026 02:43Shirika la Amnesty International mapema jana Alhamisi lilitoa wito wa kufanyika uchunguzi kuhusu mashambulizi matatu yaliyofanywa na utawala wa Israel kusini mwa Lebanon mwezi Machi, likiyataja mashambulizi hayo kuwa ni uhalifu wa kivita.
-
Rais Pezeshkian na Waziri Mkuu wa Iraq waongoza mapokezi ya mwili wa Kiongozi Shahidi mjini Najaf
Jul 08, 2026 04:49Rais Masoud Pezeshkian na Waziri Mkuu wa Iraq, Ali al-Zaidi, wamehudhuria hafla rasmi ya mapokezi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Najaf, kwa ajili ya kupokea mwili wa Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, kabla ya kuanza kwa taratibu za mazishi nchini Iraq.
-
Harakati ya Ansarullah yalaani vitisho vya muungano wa Saudi Arabia; yasema ni ishara ya kushindwa Riyadh
Jul 05, 2026 11:04Kiongozi mwandamizi wa Harakati ya Muqawama ya Ansarullah ya Yemen amelaani vitisho vya hivi karibuni vya muungano unaoongozwa na Saudi Arabia dhidi ya Yemen, akisema kuwa vinafichua kufeli Riyadh kisiasa na kijeshi pamoja na kushindwa kwake kusambaratisha mapambano ya Yemen licha ya nchi hiyo kuathirikwa kwa miaka mingi na vita na mzingiro.
-
Dakta Abu Safiya anakabiliwa na hali mbaya katika gereza la Israel
Jul 05, 2026 11:00Shirika la Kimataifa la Haki za binadamu limearifu kuwa Dakta Hussam Abu Safiya, Mkurugenzi wa Hospitali ya Kamal Adwan huko Gaza ambaye amekuwa mikononi mwa Israel tangu mwaka 2024 anakabiliwa na tishio kubwa kwa maisha yake.
-
Korea Kaskazini yalifanyia majaribio kombora la kimkakati la kruzi na silaha nyingine
Jul 05, 2026 10:57Korea Kaskazini imelifanyia jaribio kombora la kimkakati la kruzi na silaha nyingine kutoka katika meli yake mpya ya kivita ya Kang Kon yenye yenye uzito wa tani 5,000 na refu wa mita 140. Shirika Kuu la Habari la Korea Kaskazini KCNA leo limetangaza kuwa Kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong Un alisimamia majaribio hayo siku ya Ijumaa.
-
Hamas: Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa' ilibadilisha milinganyo yote ya kisiasa na kijeshi
Jul 05, 2026 03:46Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano ya Kisiasa na Vyombo vya Habari cha Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) nchini Lebanon amesema kuwa 'Operesheni ya 'Kimbunga cha Al-Aqsa' ilibadilisha milinganyo yote ya awali ya kisiasa na kijeshi, huku akisisitiza kuwa istiqama na mapambano ya taifa la Palestina vinapaswa kuenziwa kwa siku 1,000 baada ya kuanza operesheni hiyo kubwa dhidi ya Israel.
-
Umoja wa Mataifa watahadharisha juu ya janga la haki za binaadamu al-Obeid
Jul 04, 2026 04:12Mkuu wa shirika la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa Volker Turk ametahadharisha juu ya janga jingine la haki za binaadamu katika mji wa al-Obeid, nchini Sudan na kuutolea wito ulimwengu kuchukua hatua haraka iwezekanavyo.
-
Iran yaonya mataifa ya Ghuba ya Uajemi baada ya kikao kilichosimamiwa na Marekani nchini Bahrain
Jul 03, 2026 09:00Iran imetoa onyo kwa nchi za kikanda kuwa zichukue tahadhari ya juu dhidi ya mipango ya usalama inayoongozwa na Marekani, ikisema kuwa nchi hizo zisizahau athari za uvamizi wa kijeshi wa hivi karibuni wa Marekani na Israel uliovuruga usalama katika ukanda mzima wa Asia Magharibi.