-
"Ni muhali kufikia amani na Israel madhali inakiuka haki za Wapalestina"
Feb 16, 2026 06:47Waziri wa Mambo ya Nje na Wahamiaji wa Palestina, Varsen Aghabekian Shahin amesema kufikia amani na Israel "haiyumkiniki" madhali haki za Wapalestina zinakiukwa na utawala huo wa Kizayuni, akisisitiza kwamba sheria za kimataifa zinapasa kuzingatiwa, na uchukuaji wa hatua za upande mmoja lazima ukomeshwe.
-
Palestina yapongeza matokeo ya mkutano wa kilele wa Afrika uliounga mkono uanachama wake UN
Feb 16, 2026 02:28Palestina imekaribisha matokeo ya mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika uliofanyika Addis Ababa, ambao umesisitiza tena upinzani wa bara hilo dhidi ya mipango ya kuwafukuza Wapalestina katika nchi yao na kuunga mkono suala la Palestina kupata uanachama kamili katika Umoja wa Mataifa.
-
Msemaji wa serikali ya Afghanistan: Tutaiunga mkono Iran kama itakabiliwa na uadui
Feb 16, 2026 02:25Msemaji wa serikali ya Afghanistan amesisitiza kwamba watu wa Afghanistan wataonyesha mshikamano na kutoa aina mbalimbali za misaada kwa Iran iwapo kutatokea uchokozi wowote dhidi ya nchi hiyo.
-
Palestina yataka uingiliaji kati wa walimwengu kusitisha mashambulizi ya Israel
Feb 16, 2026 00:01Mamlaka ya Ndani ya Palestina, imetoa radiamali kwa uamuzi wa baraza la mawaziri la utawala wa Kizayuni wa Israel kuhusu kutaifisha ardhi za Ukingo wa Magharibi na kuitaka jamii ya kimataifa kuchukua hatua kuhusu suala hilo.
-
Wapalestina 10 wauawa katika mashambulizi ya Israel Gaza licha ya usitishaji vita
Feb 15, 2026 23:27Vikosi vya Israel vimewaua angalau Wapalestina 10 katika mashambulizi mapya yaliyofanywa katika maeneo mbalimbali ya Ukanda wa Gaza, katika ukiukaji mwingine wa makubaliano ya usitishaji vita yaliyoratibiwa na Marekani na kuanza kutekelezwa Oktoba 10 mwaka jana.
-
Mvutano waongezeka kati ya Netanyahu na Herzog baada ya Trump kumtusi Rais wa Israel
Feb 15, 2026 08:03Hatua ya Rais Donald Trump wa Marekani ya kumtusi Rais wa utawala wa kizayuni wa Israel akimuunga mkono waziri mkuu wa utawala huo yameongeza mvutano kati ya Netanyahu na Isaac Herzog.
-
Katibu Mkuu wa Hizbollah: Iran daima imekuwa ikiunga mkono Palestina na wanyonge duniani
Feb 15, 2026 07:29Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Hizbollah ya Lebanon amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imekuwa ikiunga mkono Palestina na watu wanaokandamizwa duniani.
-
"Hatuui tu, tunabaka": Mwanajeshi wa Israel aliyeua watu Gaza akiri kufanya uhalifu
Feb 15, 2026 06:54Mwanajeshi mmoja katika jeshi la Israel ametoa kauli ya kushtua katika mahojiaano ya moja kwa moja na YouTuber wa Marekani, akizungumzia vitendo vinavyofanywa na wanajeshi wa utawala huo dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza katika vita vya mauaji ya kimbari.
-
Israel yakasirishwa na kauli ya kumdhalilisha rais wake iliyotolewa na Trump
Feb 14, 2026 23:56Duru zilizo karibu na rais wa utawala wa kizayuni wa Israel zimeyaelezea matamshi ya Rais wa Marekani Donald Trump ya kumtusi na kumdhalilisha rais wa utawala huo Isaac Herzog kuwa ni uvukaji mistari myekundu.
-
Ripota maalumu wa UN: Hujuma dhidi yangu si chochote kulinganisha na mateso ya Wapalestina
Feb 14, 2026 06:26Francesca Albanese, Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya haki za binadamu katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu amesema, analengwa na hujuma za kumchafulia jina na kumtaja kwa ubaya kwa sababu ya kulaani vita vya utawala wa kizayuni wa Israel dhidi ya Ghaza na Ukingo wa Magharibi.