-
Mazoezi ya pamoja ya kijeshi kati ya China, Iran na Russia yaanza katika Bahari ya Oman
Mar 15, 2023 04:28Wizara ya Ulinzi ya China imetangaza kuwa, mazoezi ya pamoja ya kijeshi ya majini yanayoishirikisha nchi hiyo, Iran na Russia yatafanyika katika Bahari ya Oman kuanzia leo Jumatano hadi Machi 19.
-
Katibu Mkuu wa Arab League: Kupatana Tehran na Riyadh ni hatua chanya kwa maana halisi
Mar 15, 2023 04:08Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu amesema makubaliano yaliyofikiwa kati ya Iran na Saudi Arabia ni hatua nzuri na chanya kwa maana yake halisi na akaongeza kuwa athari zake za kwanza ni kupatikana kwa namna fulani utulivu wa kisiasa na kiusalama kati ya nchi hizo mbili.
-
Umoja wa Mataifa: Jamii ya kimataifa imewatelekeza wahanga wa tetemeko la ardhi nchini Syria
Mar 14, 2023 08:16Tume ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa imetangaza kuwa jamii ya kimataifa haikuchukua hatua za haraka za kupeleka misaada kwa wahanga wa tetemeko la ardhi nchini Syria.
-
Barghouthi: Hitilafu zinazoizonga Israel zinadhihirisha kiwango cha ufashisti na ubaguzi wa utawala huo
Mar 13, 2023 22:38Katibu Mkuu wa Harakati ya Ubunifu wa Kitaifa ya Palestina amesisitiza namna hitilafu na migawanyiko inayoikabili Israel sasa inavyodhihirisha kwa walimwengu kiwango cha ufashisti na ubaguzi wa utawala huo ghasibu na kueleza kuwa muqawama wa Palestina unaweza kustafidi na fursa ya mfarakano huu unaoukabili utawala wa Kizayuni.
-
Taathira za kuimarishwa uhusiano wa Iran na Saudi Arabia kwa utawala wa Kizayuni
Mar 13, 2023 22:35Baada ya miaka 7 ya kuvunjwa uhusiano wao, Iran na Saudi Arabia zilitia saini taarifa ya kurejesha uhusiano kwa upatanishi wa China mnamo Machi 10 huko Beijing. Kwa mujibu wa taarifa hiyo, balozi za nchi hizi mbili zitafunguliwa baada ya miezi miwili.
-
Kiongozi wa HAMAS: Makubaliano ya Iran na Saudia ni kwa manufaa ya muqawama
Mar 13, 2023 09:19Dr. Mahmoud al-Zahar, kiongozi mwandamizi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesema kuwa, makubaliano ya Iran na Saudi Arabia ni kwa maslahi ya muqawama na kwamba, harakati hiyo inayaunga mkono.
-
Afisa wa jeshi la Iraq: Zaidi ya wanachama 400 wa ISIS bado wako Iraq
Mar 13, 2023 03:53Afisa wa jeshi la Iraq amesema kuwa kundi la kigaidi la Daesh (ISIS) bado lina wapiganaji 400 hadi 500 katika nchi hiyo.
-
Sababu za Saudia kufikia makubaliano na Iran
Mar 13, 2023 02:51Iran na Saudi Arabia zimekubaliana kurejesha uhusiano wao wa kidiplomasia baada ya kukatwa kwa miaka 7 na kuamua kufungua tena balozi zao katika muda wa miezi miwili ijayo.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudia: Nina hamu ya kuonana na waziri mwenzangu wa Iran
Mar 13, 2023 02:19Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia, Faisal bin Farhan ameelezea nia yake ya kukutana haraka na Waziri mwenzake wa Mambo ya Nje wa Iran, Hossein Amir-Abdollahian, baada ya nchi hizi mbili kufikia makubaliano ya kufufua uhusiano baina yao.
-
Libya: Mapatano kati ya Iran na Saudi Arabia ni kwa maslahi ya nchi za Asia Magharibi
Mar 12, 2023 23:12Wizara ya Mambo ya Nje ya Libya imetoa taarifa na kukaribisha mapatano yaliyofikiwa kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Saudi Arabia na kueleza kuwa, mapatano hayo yana maslahi kwa nchi mbili na eneo zima la Asia Magharibi kwa ujumla.