-
Kambi ya jeshi ya Marekani yashambuliwa kwa droni nchini Syria
Jan 21, 2023 06:52Kamandi Kuu ya Jeshi la Marekani (CENTCOM) imekiri kuwa, moja ya kambi za kistratejia za nchi hiyo huko kusini mwa Syria imeshambuliwa kwa ndege zisizo na rubani (droni).
-
Wapalestina 75,000 washiriki katika Sala ya Ijumaa kwenye Kibla cha Kwanza cha Waislamu
Jan 21, 2023 02:59Makumi ya maelfu ya Waislamu wa Palestina jana walishiriki katika ibada ya Sala ya Ijumaa kwenye Kibla cha Kwanza cha Waislamu yaani Msikiti wa al Aqsa, licha ya vikwazo vingi vya utawala wa Kizayuni.
-
Walowezi wa Kizayuni wavamia Msikiti wa al-Aqsa katika muendelezo wa uchochezi
Jan 20, 2023 23:46Makumi ya walowezi Waisraeli wamevamia eneo la Msikiti wa al-Aqsa huko Quds (Jerusalem) Mashariki inayokaliwa kwa mabavu na utawala haramu wa Israel, katika hatua nyingine ya uchochezi dhidi ya waumini Waislamu wa Kipalestina.
-
Kuongezeka juhudi za wapatanishi kwa ajili ya kusitisha vita Yemen
Jan 20, 2023 22:55Juhudi za pande za kigeni kwa ajili ya kufanikisha usitishaji vita huko Yemen zimeongezeka sambamba na kuanza mwaka huu mpya wa Miladia.
-
Uungaji mkono kwa taifa madhulumu la Palestina washamiri Amerika ya Latini katika mji mkuu wa Colombia
Jan 20, 2023 04:00Baraza la Manispaa la Bogotá, mji mkuu wa Jamhuri ya Colombia, limebadilisha jina la moja ya mitaa muhimu ya jiji hilo kuuita "Mtaa wa Nchi ya Palestina".
-
Bunge la Lebanon lakwama kwa mara ya 11 kumchagua Rais mpya
Jan 19, 2023 23:16Bunge la Lebanon jana lilikwama tena kumchagua Rais mpya wa nchi hiyo na kupelekea mkwamo wa kumchagua kiongozi wa juu zaidi nchini humo kuendelea kushuhudiwa.
-
Israel yashadidisha ukatili wake dhidi ya Wapalestina Ukingo wa Magharibi
Jan 19, 2023 06:56Wanajeshi makatili wa utawala wa Kizayuni wa Israel wameshambulia kambi ya wakimbizi ya Wapalestina katika mji wa Jenin, kaskazini mwa eneo la Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan linalokaliwa kwa mabavu, na kuua shahidi Wapalestina wawili.
-
Januari 19; Siku ya Ghaza na nembo ya muqawama wa Kiislamu
Jan 19, 2023 06:36Januari 19 imetajwa katika kalenda ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa ni "Siku ya Ghaza" kwa mnasaba wa kumbukumbu ya vita vya siku 22 katika Ukanda wa Ghaza huko Palestina.
-
China: Marekani ni wavamizi, wahalifu na wanapora kidhulma mafuta ya Syria
Jan 19, 2023 03:20Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China amelalamikia vikali uhalifu unaoendelea kufanywa na Marekani nchini Syria na kusema kuwa, vitendo hivyo vya Wamarekani ni wizi, ni uhalifu wa kinyama na ni uporaji wa mchana kweupe wa maliasili ya Syria.
-
Kwa mnasaba wa Siku ya Gaza, Waarabu watakiwa kuwa bega kwa bega na Muqawama kama ilivyo Iran
Jan 18, 2023 23:32Msemaji wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema, Iran inaunga mkono kishujaa kadhia na piganio tukufu la Palestina; na inavyotarajiwa, nchi za Kiarabu nazo pia zichukue msimamo kama huo wa Tehran.