-
Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu yasisitiza kuunga mkono haki za Wapalestina
Nov 02, 2022 10:10Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imesisitiza kuendelea kutetea na kuuunga mkono haki za wananchi madhulumu wa Palestina.
-
Walebanon wataka kutimuliwa balozi wa Saudi Arabia mjini Beirut
Nov 02, 2022 10:09Wananchi wa Lebanon wametoa mwito wa kutimuliwa nchini humo balozi wa Saudi Arabia wakimtuhumu kwamba, amekuwa akiingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo.
-
Uchaguzi wa tano wa bunge la Israel katika muda wa chini ya miaka minne
Nov 02, 2022 04:50Uchaguzi wa tano wa bunge la Israel katika muda wa chini ya miaka minne ulifanyika jana Jumanne tarehe 1 Novemba.
-
Ukiukwaji wa haki za binadamu; ombi la makundi ya kutetea haki za binadamu kwa Papa
Nov 02, 2022 04:35Taasisi 9 za kutetea haki za binadamu zimetangaza kuwa, Papa Francis Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani akiwa ziarani huko Bahrain anapasa kutoa wito kwa watawala wa nchi hiyo ili wakomeshe hatua zao za kukiuka haki za binadamu.
-
Qatar yataka kuhitimishwa ukaliaji mabavu wa utawala wa Kizayuni
Nov 02, 2022 04:29Mwakilishi wa Kudumu wa Qatar katika Umoja wa Mataifa leo asubuhi amehutubia katika kikao cha kiduru cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kusema: Israel inapasa kuhitimisha hatua zake za kuzikalia kwa mabavu ardhi za Waarabu ikiwemo miinuko ya Golan huko Syria, ardhi za Lebanon na Palestina.
-
Ulazima wa utawala wa Kizayuni wa Israel wa kujiunga na mkataba wa NPT
Nov 01, 2022 22:53Kamati ya Kwanza ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa imepasisha kwa wingi wa kura muswada wa Misri unaoelezea ulazima wa utawala haramu wa Israel kujiunga na Mkataba wa Kuzuia Uzalishaji na Usambazaji wa Silaha za Atomiki (NPT).
-
Watu 53 wasubiri kunyongwa kwa umati Saudia, Magharibi kimya! + VIDEO
Nov 01, 2022 07:47Nchi za Magharibi zimeendelea kunyamazia kimya taarifa kuwa Saudi Arabia imepanga kuwanyonga kwa umati watu 53 nchini humo. Kwa uchache wanane kati ya watu hao ni watoto wadogo.
-
Kwa mara nyingine Yemen yawaonya wavamizi wasipore utajiri wa nchi hiyo
Nov 01, 2022 07:31Waziri wa Mambo ya Nje wa Serikali ya Wokovu wa Kitaifa ya Yemen yenye makao yake makuu mjini San'a amezionya nchi vamizi ziache kupora utajiri wa nchi hiyo.
-
Saudia yalaumiwa vikali kuruhusu tamasha la Halloween na kuvunja heshima ya Haramaini
Nov 01, 2022 03:38Kusambazwa picha za tamasha la kishetani la "Halloween" katika mji mkuu wa Saudi Arabia Riyadh kwa usaidizi na uungaji mkono wa Bodi ya Burudani ya nchi hiyo kumeibua wimbi la hasira kali na kauli za kejeli kwenye mitandao ya kijamii.
-
Raia wengine 15 wakiwemo watoto 8 wahukumiwa kunyongwa nchini Saudi Arabia
Oct 31, 2022 22:59Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Kisaudia lenye makao yake barani Ulaya limefichua kuwa, viongozi wa Riyadh wamewahukumu adhabu ya kunyongwa wafungwa 15 wa kisiasa wakiwemo watoto kadhaa wadogo.