Russia: Kujisalimisha ndilo chaguo pekee lililosalia kwa Ukraine
https://parstoday.ir/sw/news/world-i101010-russia_kujisalimisha_ndilo_chaguo_pekee_lililosalia_kwa_ukraine
Naibu wa Baraza la Usalama la Russia amesema kuwa mashambulizi ya Ukraine ya kukabiliana na Russia yanapeleka maelfu ya watu machinjioni, na jambo pekee ambalo Ukraine inahitaji leo ni kusitisha mapigano.
(last modified 2025-11-07T02:31:33+00:00 )
Aug 13, 2023 08:20 UTC
  • Russia: Kujisalimisha ndilo chaguo pekee lililosalia kwa Ukraine

Naibu wa Baraza la Usalama la Russia amesema kuwa mashambulizi ya Ukraine ya kukabiliana na Russia yanapeleka maelfu ya watu machinjioni, na jambo pekee ambalo Ukraine inahitaji leo ni kusitisha mapigano.

Kulingana na shirika la habari la TASS, Dmitry Medvedev, Naibu wa Baraza la Usalama la Russia, ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa Telegraph: "Watu ambao wanateseka kwenye handaki za nchi iliyogawanyika na iliyofarikiana wanahitaji kujisalimisha, na baada ya hapo njia kwa amani itapatikana. Lakini ieleweke kwamba si Washington wala Kiev inayotaka amani."

Rais huyo wa zamani wa Russia amefananisha mashambulizi ya Ukraine na "kiwanda cha kusindika nyama" na kusisitiza kuwa kiwanda hiki "sasa kinafanya kazi bila kukoma, na kupeleka maelfu ya watu wenye bahati mbaya kwenye machinjio."

Medvedev ameashiria ombi la hivi karibuni la userikali ya Rais wa Marekani, Joe Biden kwa Bunge la nchi hiyo la kutenga dola bilioni 13 kwa ajili ya Ukraine kama msaada wa dharura wa kijeshi, na kusema: Dunia iliyo macho kwa mara nyingine tena imeshtushwa baada ya kusikia habari za kutengwa makumi ya mabilioni ya dola zisizo na faida kwa mazombi wa nchi 404. 

Nchi za Ulaya na Magharibi, hasa Marekani, zinachochea zaidi moto wa vita na mapigano katika nchi ya Ukraine kwa kuzidisha shinikizo la vikwazo dhidi ya Shirikisho la Russiia na kutuma aina mbalimbali za silaha nyepesi na nzito kwa serikali ya Kiev.