Waafrika wasisitiza umuhimu wa Siku ya Kimataifa ya Quds
https://parstoday.ir/sw/news/world-i10174-waafrika_wasisitiza_umuhimu_wa_siku_ya_kimataifa_ya_quds
Shakhsia mbalimbali wa Kiafrika wameendelea kutilia mkazo umuhimu wa kufanyika kwa mafanikio na adhama kubwa shughuli za Siku ya Kimataifa ya Quds.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 28, 2016 09:40 UTC
  • Waafrika wasisitiza umuhimu wa Siku ya Kimataifa ya Quds

Shakhsia mbalimbali wa Kiafrika wameendelea kutilia mkazo umuhimu wa kufanyika kwa mafanikio na adhama kubwa shughuli za Siku ya Kimataifa ya Quds.

Mratibu wa Muungano wa Mabaraza ya Kutetea Haki za Binadamu nchini Morocco, Abdul Razzaq Bughanbur amesema kuwa Siku ya Kimataifa ya Quds iliyotangazwa na mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hayati Imam Khomeini kwa Waislamu wote, imewafanya Waislamu watafakari kuhusu mchango wao katika kulinda Quds tukufu. Bughanbur ameongeza kuwa, Waislamu wote duniani wanapaswa kufanya jitihada kubwa za kuhuisha mpango wa kukomboa Quds tukufu.

Naye Rumani Jadallah ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa Kituo cha Haki za Binadamu cha al Kalimah nchini Misri amewataka Waislamu kubakisha hai Siku ya Kimataifa ya Quds na kusema: Imam Ruhullah Khomeini alielewa kwamba Quds itakuja kukombolewa na kwa msingi huo aliwahamasisha Waislamu na kuwapa matumaini ya kukombolewa kibla chao cha kwanza.

Ijumaa ya mwisho la kila mwezi mtukufu wa Ramadhani ilitangazwa na mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hayati Imam Khomeini kuwa ni Siku ya Kimataifa ya Quds na kuwataka Waislamu kote duniani kuonesha hasira yao dhidi ya maghasibu Wazayuni wa Israel na siasa zao za kibaguzi.