Frontex: Wakimbizi wanazidi kumiminika Ulaya kupitia Misri
Shirika la Frontex limeripoti kuwa, lina wasiwasi kuhusu ongezeko kubwa la wakimbizi kuingia barani Ulaya kwa kupitia Misri na kwamba wakimbizi hao wanakabiliwa na hatari ya kifo baharini.
Mkurugenzi wa shirika la Frontex linalosimamia mipaka ya Ulaya, Fabrice Leggeri amesema kuwa, Misri imekuwa njia ya wakimbizi kuingia Ulaya na mwanzo wa safari yenye hatari kubwa kwa maisha ya wakimbizi hao.
Afisa huyo wa Ulaya amesema kuwa, tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa 2016 wakimbizi karibu elfu moja walielekea Italia kutokea Misri kwa kutumia boti zisizo salama za magenge ya wafanya magendo ya binadamu.
Fabrice Leggeri ametahadharisha kuwa, safari hiyo ya siku kumi huambatana na hatari kubwa na kughiriki boti zinazotorosha wakimbizi hao.
Maelfu ya wakimbizi kutoka nchi zilizoathiriwa na vita za Mashariki ya Kati na Afrika wamekuwa wakiingia barani Ulaya na maelfu ya wengine kughariki baharini katika jitihada zao za kufika pwani ya Ulaya.