Oct 21, 2023 07:24 UTC
  • Ukosoaji wa Russia kwa siasa za uadui za Marekani ulimwenguni

Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Kitaifa la Russia amekosoa vikali siasa za uhasama za Marekani ulimwenguni.

Kwa mujibu wa shirika la habari la TASS, Dmitry Medvedev, Naibu Mkuu wa Baraza la Usalama la Kitaifa la Russia, huku akikosoa siasa za uchokozi na uadui za Marekani duniani, amesema kwamba Marekani inaisukuma dunia katika shimo kubwa.

Dmitry Medvedev pia amesema kuwa maamuzi yanayochukuliwa na viongozi wa Marekani yanaonyesha wazi kwamba sio tu kuwa wana maradhi ya akili, bali pia wamevuka mipaka ya mwisho ya maadili. Maria Zakharova, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia, pia alisema awali kwamba Marekani imeifanya hali ya usalama katika Asia Magharibi kuwa mbaya sana.

Amesema siasa za  nje za Marekani wakati wa uongozi wa  Rais Joe Biden, zimevuruga juhudi za kufikiwa makubaliano na kuisukuma dunia kwenye ukingo wa vita kwa kuharibu hali ya Ulaya, eneo la Asia-Pacific, Afrika na Asia Magharibi.

Tags