Magaidi wa ISIS waua watu 22 mgahawani Bangladesh
https://parstoday.ir/sw/news/world-i10453-magaidi_wa_isis_waua_watu_22_mgahawani_bangladesh
Magaidi wakufurishaji wa kundi la ISIS (Daesh) wameua watu wasiopungua 22 katika ufyatuaji risasi uliojiri Ijumaa usiku mgahawani katika mji mkuu wa Bangladesh, Dhaka.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jul 02, 2016 13:44 UTC
  • Magaidi wa ISIS waua watu 22 mgahawani Bangladesh

Magaidi wakufurishaji wa kundi la ISIS (Daesh) wameua watu wasiopungua 22 katika ufyatuaji risasi uliojiri Ijumaa usiku mgahawani katika mji mkuu wa Bangladesh, Dhaka.

Polisi wanasema mateka 13 waliokolewa katika mgahawa wa Holey Artisan Bakery mjini Dhaka huku kundi la ISIS lilijigamba kuwa limehusika katika umwagaji damu huo uliojiri katika eneo hilo lenye idadi kubwa ya wanadiplomasia wa kigeni. Bangladesh haijaweza kuthibitisha madai ya magaidi kuwa waliua watu 24 na kuwajeruhi wengine 40. Aidha askari wawili wa Bangladesh wanaripotiwa kuuawa katika tukio hilo. Kati ya raia wa kigeni waliouawa ni Wajapani, Wataliano, Wasirilanka na Wahindi. Vikosi vya Bangladesh vimefanikiwa kuwaua magaidi sita kati ya tisa waliotekeleza hujuma hiyo. Ripoti zinasema raia wengi wa kigeni waliouawa katika tukio hilo walikuwa wamekatawa shingo.

Waziri Mkuu wa Bangladesh, Sheikh Hasina, ameapa kukabiliana na ugaidi na ametoa wito kwa wananchi kutoa habari zitakazosaidia kuangamiza ugaidi nchini humo.