Nov 11, 2023 13:47 UTC
  • Pakistan haiiungi mkono tena serikali ya Taliban katika ngazi ya kimataifa

Kufuatia kuongezeka mivutano katika uhusiano wa Kabul na Islamabad, gazeti moja la Pakistan limeandika kuwa serikali ya nchi hiyo haiiungi mkono tena serikali ya Taliban ya Afghanistan katika ngazi ya kimataifa.

Gazeti la Pakistan la Express Tribune limeandika katika toleo lake la karibuni kuwa baada ya kuongezeka mivutano ya kiusalama katika uhusiano wa Kabul na Islamabad, Pakistan imebadilisha sera yake kuhusiana na Taliban na kuamua kutounga mkono "faili la Taliban ya Afghanistan" katika ngazi ya kimataifa.
 
Express Tribune limedai kuwa mabadiliko ya sera ya Pakistan kuhusu Taliban yamepunguza uwezekano wa serikali ya kundi hilo kutambuliwa katika ngazi ya kimataifa.
Zabihullah Mujahid

Hii ni licha ya kuwa baada ya kundi la Taliban kuingia tena madarakani nchini Afghanistan mwezi Agosti 2021, Pakistan iliibuka kuwa muungaji mkono na mtetezi wa serikali ya Kabul na kuitaka jamii ya kimataifa hasa nchi za Magharibi zianzishe mawasiliano na Taliban.

 
Hata hivyo, duru za Pakistan zimeiambia The Express Tribune kwamba Islamabad haitaufanyia tena wema wowote maalumu utawala wa Taliban, kwa sababu kundi hilo limewapa hifadhi maadui wa Pakistan.
 
Kwa upande mwingine, Anwar Haq Kakar, Kaimu Waziri Mkuu wa Pakistan, naye pia alisema hapo kabla katika mkutano na waandishi wa habari kwamba baada ya Taliban kuidhibiti tena Afghanistan, matukio ya kigaidi nchini Pakistan yameongezeka kwa 60%.
 
Hata hivyo Zabihullah Mujahid, msemaji wa serikali ya Afghanistan ametoa mjibizo kwa matamshi ya viongozi wa Pakistan na kusema kuwa Wapakistani wanapaswa kutatua matatizo ya ndani ya nchi yao wao wenyewe na si kuilaumu Kabul na kuibebesha dhima ya kushindwa kwao.../

 

Tags