Nov 24, 2023 06:55 UTC
  • Makumi ya maelfu ya Wacuba waandamana kuwaunga mkono watu wa Palestina

Makumi ya maelfu ya wananchi wa Cuba wameandamana katika mji mkuu wa nchi hiyo Havana kuwaunga mkono wananchi wa Palestina.

Shirika la habari la Irna limeripoti kuwa, makumi ya maelfu ya watu jana Alhamisi waliandamana mbele ya ubalozi wa Marekani mjini Havana Cuba na kulaani maangamizi ya kizazi yanayofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina huko Gaza.  

Jinai za Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Gaza 

Maandamano hayo yaliongozwa na Rais wa Cuba Miguel Diaz-Canel na yalifanyika kando ya njia ya pwani ya Havana, yalipo makao makuu ya kidiplomasia ya Marekani. 

Washiriki katika maandamano hayo walikuwa wamebeba bendera za Palestina na mabango yenye maandishi ya kuwaunga mkono wananchi wa Palestina huku wakipiga nara kama Palestina iwe huru", "Israeli ya mauaji ya kizazi " na "Kusonga mbele kuelekea kukombolewa Palestina". 

Pamoja na kuwa Cuba haina uhusiano wa kidiplomasia na utawala wa Israel lakini nchi hiyo kwa miongo kadhaa imekuwa ikiunga mkono malengo ya Palestina na kukombolewa taifa hilo na imetoa mafunzo kwa Madaktari wa Kipalestina zaidi ya 200. 

Ante Rodríguez, mmoja wa Maprofesa wa Chuo Kikuu cha Havana, alisema jana katika maandamano hayo kuwa: "Tuko hapa na sio bahati mbaya kwamba tumeandamana mbele ya Ubalozi wa Marekani. Aidha alisisitiza  uungaji mkono wa Washington ni moja ya sababu kuu inayoupelekea utawala wa Israel kutekeleza mauaji hayo dhidi ya Wapalestina na kukiuka sheria za kimataifa.

Tags