Jan 07, 2024 12:13 UTC
  • Kiongozi wa upinzani nchini Ufaransa atoa wito wa kuvunjwa shirika la kijeshi la NATO

Kiongozi wa chama cha Wazalendo (Patriots Party) nchini Ufaransa ametoa wito wa kuvunjwa shirika la kijeshi la nchi za Magharibi la NATO ili amani iweze kudhihiri duniani.

Florian Philippot, kiongozi wa Chama cha Wazalendo wa Ufaransa, ameandika kwenye mtandao wa kijamii wa X: "NATO bila aibu imemtumia Zelensky kama kibaraka wake kuvuruga uchumi wa nchi zetu, kutuingiza kwenye umaskini na kuwasukumiza mamia ya maelfu ya watu wa Ukraine kwenye vifo visivyo na shaka na visivyo na maana!" "Lazima tuiangamize NATO kwa ajili ya amani ya dunia."
 
Tangu vilipoanza vita kati ya Russia na Ukraine mnamo Februari 24, 2022, Umoja wa Ulaya umechangia zaidi ya dola bilioni 91 kwa ajili ya Ukraine kwa anuani tofauti.

Wakati huohuo, Shalanda Young, afisa mwandamizi wa masuala ya bajeti katika serikali ya Joe Biden, ametahadharisha kuhusu ukomo wa muda walionao wabunge wa Marekani wa kupitisha bajeti ya msaada kwa Ukraine na kueleza kwamba, kwa kuzingatia uhusiano uliopo kati ya bajeti hiyo na masuala mengine ikiwa ni pamoja na makubaliano juu ya masuala ya uhamiaji, hali kwa ajili ya kuwezesha kutoa misaada hiyo ni mbaya.

 
Vita vya Ukraine vingali vinaendelea katika mwezi wake wa 23 licha ya athari zake nyingi za kisiasa, kijeshi, kiuchumi, kijamii na hata kitamaduni, huku nchi za Magharibi zikiwa zingali zinatuma shehena za silaha kwa serikali ya Kiev.
 
Nchi za Ulaya na Magharibi hususan Marekani, zinazidisha mashinikizo ya vikwazo dhidi ya Russia na kuipatia Kiev kila aina ya silaha nyepesi na nzito, hatua ambayo sio tu haijasaidia kukomesha vita vya Ukraine, bali pia imekoleza moto wa mapigano katika nchi hiyo.
 
Viongozi wa Russia na baadhi ya wataalamu na vyombo vya habari vya nchi za Magharibi wamevitaja vita vya Ukraine kuwa ni vita vya niaba kati ya Magharibi na Russia.../
 
 

Tags