Mar 04, 2024 02:28 UTC
  • Russia yatungua makumi ya droni za Ukraine

Wizara ya Ulinzi ya Russia imetangaza kuwa imezidhibiti na kuzitungua ndege kadhaa zisizo na rubani za Ukraine (Droni) katika Peninsula ya Crimea.

Shirika la habari la Sputnik limearifu kuwa, Wizara ya Ulinzi ya Russia jana Jumapili ilitoa taarifa na kutangaza kuwa kikosi cha ulinzi wa anga cha jeshi la nchi hiyo kimenasa na kuziharibu ndege zisizo na rubani 38 za jeshi la Ukraine katika eneo la Peninsula ya Crimea. 

Peninsula ya Crimea imeshambuliwa na vikosi vya Ukraine mara kadhaa hadi sasa tangu kuanza kwa vita huko Ukraine  Februari 24 mwaka 2022; mashambulizi ambayo mengi yalizuiliwa na kikosi cha ulinzi wa anga cha Russia.  

Hii ni katika hali ambayo Moscow inaihesabu Peninsula ya Crimea kuwa sehemu ya ardhi ya Russia; na imetangaza kuwa itatumia njia zote ikiwa ni pamoja na silaha za nyuklia kulinda  umoja wa ardhi wa nchi hiyo.  

Kisiwa cha Crimea kilijiunga na Russia mwaka 2014 baada ya  kura ya maoni hata hivyo Ukraine na nchi nyingine kadhaa za Magharibi hazijatambua rasmi hatua hiyo ya Crimea kujiunga na Russia  na kufanyika kura hiyo ya maoni.  

 

Tags