Apr 08, 2024 02:44 UTC
  • Waziri wa Ulinzi wa serikali ya Obama: Waisraeli kwanza wanafyatua risasi,  kisha wanauliza maswali!

Waziri wa Ulinzi wakati wa utawala wa Barack Obama Rais mstaafu wa Marekani amesema kuwa haishangazi kwamba Waisraeli wamekiri makosa yao baada ya shambulio la hivi karibuni na mauaji dhidi ya watoa misaada wa kimataifa wa shirika la World Central Kitchen (WCK), kwa sababu kwa kawaida wao kwanza hupiga risasi na kisha huuliza maswali!

Leon Panneta aliyekuwa Waziri wa Ulinzi wa Marekani katika utawala wa Barack Obama ambaye pia ni mkuu wa zamani wa Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) amesema katika mahojiano na televisheni ya CNN kuwa: "Inabidi kuchukua muda ili kuhakikisha kuwa habari unayopata inahusu malengo sahihi, lakini sivyo ilivyo kwa Waisraeli, kwa sababu, kutokana na uzoefu uliopo, kwanza huwa wanapiga risasi na baadaye ndipo huuliza maswali.

Waziri huyo wa zamani wa ulinzi wa Marekani ameeleza haya ikiwa zimepita siku kadhaa tangu jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel litekeleza mauaji dhidi ya msafara wa wafanyakazi wa World Central Kitchen huko Ukanda wa Gaza. 

Utawala wa Kizayuni siku kadhaa zilizopota uliishambulia gari ya wafanyakazi wa WCK katika eneo la Deir al Balah ambako walikuwa wakigawa chakula kwa wakimbizi wa Kipalestina. Katika hujuma hiyo wafanyakazi saba wakiwemo raia sita wa kigeni waliuawa. 

Wafanyakazi wa WCK waliouliwa katika shambulio la anga la Israel 

 

Tags