Russia: Marekani badala ya kushupalia Ukraine iimarishe usalama wake wa ndani
-
Maria Zakharova
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Russia amesitiza baada ya Donald Trump kupigwa risasi kwenye kampeni ya uchaguzi kwamba Marekani inapaswa "kupima" sera zake za "uchochezi wa chuki".
Maria Zakharova msemaji wa Wizara ya Mashauuri ya Kigeni ya Russia amesema msaada wa Marekani kwa Ukraine unatumiwa kuchochea mashambulizi dhidi ya rais wa Russia na badala yake akapendekeza Marekani kuwekeza zaidi katika usalama wa ndani.
Bi Maria Zakharova amesisitiza kuwa, "Pengine pesa hizi zingetumika vyema kufadhili polisi wa Marekani na huduma zingine ambazo zinapaswa kuhakikisha sheria na utulivu upatanikana nchini Merekani.
Raisi wa zamani wa Marekani, Donald Trump, na mgombea wa sasa wa kiti cha rais nchini humo juzi alijeruhiwa kwa risasi akiwa katika mkutano wa hadhara huko Butler, katika jimbo la Pennsylvania akihutubia wafuasi wake; hatua iliyoipelekea timu yake ya ulinzi kumtoa katika sehemu ya tukio.

Idara ya Upelelezi ya Marekani (FBI) imethibitishai kwamba shambulizi dhidi ya rais wa zamani na mgombea wa sasa, Donald Trump, huko Pennsylvania kwamba, lilikuwa jaribio la mauaji, na kwamba imemtambua mpiga risasi aliyeuawa, huku uchunguzi ukiendelea.
Idara ya Upelelezi ya Marekani imesisitiza kwamba, inaendelea kufanya uchunguzi na upekuzi wa maeneo yanayotiliwa shaka, magari na maeneo yanayohusiana na tukio hili.
Video ya moja kwa moja kutoka eneo la tukio ilimuonyesha Trump akivuja damu upande wa kulia wa uso na sikio lake. Trump alionekana akiweka mkono wake sikioni kabla ya kuanguka chini nyuma ya jukwaa.