Kukosoa Russia upinzani wa Magharibi kwa muundo mpya wa ulimwengu
Balozi wa Russia nchini Marekani, Anatoly Antonov, amesema nchi za Magharibi zinapinga juhudi za kuundwa muundo mpya wa pande kadhaa ambao utakuwa na insafu na uadilifu zaidi.
Katika makala kwa Taasisi ya Ujerumani ya Schiller, Antonov ameandika: Russia ni mfuasi wa kuundwa muundo wa kimataifa wa pande kadhaa ambao utakuwa thabiti zaidi na unaozingatia hati ya Umoja wa Mataifa na kanuni ya usawa wa mamlaka ya mataifa.
Balozi wa Russia nchini Marekani, Anatoly Antonov amesisitiza kwa kusema kwamba, kundi la Magharibi bado linapinga juhudi hizi na linajaribu "kukabiliana na nguvu" ili kudumisha hadhi yake kama "bwana wa hatima" ya wengine.
Hatua ya Russia ya kukosoa mtazamo hasi wa nchi za Magharibi kwa uongozi wa Marekani dhidi ya kuundwa mfumo na muundo mpya wa dunia unaoegemezwa kwenye misingi ya pande nyingi inapata maana zaidi hasa kwa kuzingatia misimamo na vitendo vya madola ya Magharibi vya kuzuia kuanzishwa muundo mpya wa uongozi wa ulimwengu.
Wamagharibi wamejitokeza mara chungu nzima na kutangaza wasiwasi mkubwa walionao wa kubadilishwa nidhamu na mfumo wa uongozi wa dunia wa kiliberali ambao una msingi wa thamani za Kimagharibi.
Miongoni mwao ni mkurugenzi wa taasisi ya kiintelijensia ya Marekani ambaye Machi mwaka huu aliakisi katika ripoti yake ya kila mwaka kile alichokiita vitisho vinavyoukabili ulimwengu. Katika ripoti hiyo kulielezwa wasiwasi wa vyombo vya usalama vya nchi hiyo kuhusu hatari za kiusalama zinazoikabili Washington. Ripoti hiyo ilibainisha juhudi za nguvu mpya hususan China, kubadilisha utaratibu wa dunia.
Ripoti hiyo inasema kuwa; "madola makubwa, na mamlaka zenye nguvu zinazoibuka za kikanda, na watendaji wasio wa serikali wanafuatilia suala la kuwa na satwa katika mfumo wa utawala wa dunia na watashindana katika kuandaa mazingira na kutunga sheria ambazo zitaunda utaratibu huo kwa miongo kadhaa ijayo.
Ripoti hiyo inaeleza kuwa ushindani wa kimkakati kati ya Marekani na washirika wake; na vile vile China na Russia kuhusu aina ya dunia itakayojitokeza una umuhimu mkubwa katika kubainisha ni nani na nini kitachangia masimulizi kuhusiana na hatua za Russia nchini Ukraine.
Katika hotuba yake kwenye Mkutano wa Usalama wa Munich mnamo Februari 2022, Josep Borrell mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya, alichukua msimamo mkali dhidi ya Russia na China na kutaka kukabiliana na mataifa haya mawili ya kimataifa na kulinda "kigezo cha demokrasia ya Magharibi."
Kuongezeka kwa ushirikiano na ushiriki wa madola yanayoibukia siku zote kumekuwa kukikabiliwa na majibu hasi ya kambi ya Magharibi kwa uongozi wa Marekani.
Marekani ambayo ina wasi wasi kuhusu ongezeko la mara kwa mara la nguvu na ushawishi wa kikanda na kimataifa wa nchi hizo hususan China na Russia, imefanya kila jitihada kuwasilisha taswira ya kutisha ya madola haya mawili ya Mashariki na Eurasia, ambayo inaweza kuitwa kuwa ni chuki dhidi ya China (Sinophobia) na Russia (Russophobia).