Mkuu wa Sera za Nje wa EU atoa taarifa kuhusu Syria
Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya ametangaza kuwa kipaumbele cha Ulaya ni kuhakikisha amani inakuwepo katika eneo na kwamba umoja huo utashirikiana na wadau wote katika eneo zima ikiwemo Syria katika uwanja huo.
Kaja Kallas ameeleza kuwa Umoja wa Ulaya hautachukua uamuzi wa kuondoa vikwazo dhidi ya Syria hadi pale utakapohakikisha kuwa serikali mpya inalinda haki za walio wachache na wanawake nchini humo.
Mwanadiplomasia huyo mkuu wa Umoja wa Ulaya alisema wiki iliyopita katika kikao cha kamati ya bunge ya Umoja wa Ulaya kuwa kuna wasiwasi kuhusu hatari ya kuibuka machafuko ya kimapote huko Syria na kuibuka upya mielekeo ya uchupaji mipaka nchini humo.
Mnamo Novemba 27 mwaka huu, magaidi na wapinzani wanaobeba silaha huko walianzisha hujuma kubwa dhidi ya ngome na kambi za jeshi la Syria katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo ambazo hatimaye zilipelekea kuondolewa madarakani siku ya Jumapili Disemba 8 serikali ya Rais wa nchi hiyo Bashar al Assad.