Bunge la Uhispania lahimizwa kuvunja uhusiano wa kidiplomasia na Israel
Jukwaa jipya lililoundwa kwa jina la Wanasheria wa Palestina linalojumuisha mawakili, majaji, waendesha mashtaka na wanasomi mbalimbali limetaka Kongresi ya Uhispania kuunga mkono pendekezo la kukata uhusiano wa kidiplomasia na Israel na kuuwekea vikwazo utawala huo vamizi unaozikalia kwa mabavu ardhi za Palestina.
Msemaji wa kongamano hilo Hakimu Pilar Barrado aliangazia kuwa pendekezo hilo lililoidhinishwa na takriban wataalamu 1000 wa sheria na kuitaka serikali ya Uhispania kuzingatia mikataba na maazimio ya kimataifa yaliyowasilishwa na mahakama ya ICJ na Umoja wa Mataifa.
Hakimu Barrado amesema kuwa kongamano lao linataka kusitishwa uhusiano wa kibiashara kati ya Uhispania na utawala wa Israel ambao ambayo unaendelea kuvamia maeneo mbalimbali ya Palestina, na linataka kuchukuliwa hatua, ikiwa ni pamoja na kuwekewa vikwazo viongozi wa Israel wanaohusika na mashambulizi ya Gaza.
Wanasheria hao wa Uhispania wanaitaka serikali ya nchi hiyo kushirikiana na Umoja wa Mataifa ili kufanikisha usitishaji vita Ukanda wa Gaza, ambao utawezesha usambazaji wa misaada ya kibinadamu na kurejesha huduma za kimsingi kwa wakazi wa eneo hilo.