Trudeau: Canada haitakuwa jimbo la 51 la Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i121380-trudeau_canada_haitakuwa_jimbo_la_51_la_marekani
Waziri Mkuu wa Canada ambaye ataondoka madarakani mwezi Machi mwaka huu amesema kuwa mazungumzo kuhusu kuibadilisha Canada na kuwa jimbo la 51 la Marekani hayatafanikiwa.
(last modified 2025-01-13T07:18:58+00:00 )
Jan 13, 2025 07:18 UTC
  • Trudeau: Canada haitakuwa jimbo la 51 la Marekani

Waziri Mkuu wa Canada ambaye ataondoka madarakani mwezi Machi mwaka huu amesema kuwa mazungumzo kuhusu kuibadilisha Canada na kuwa jimbo la 51 la Marekani hayatafanikiwa.

Justin Trudeau Waziri Mkuu wa Canada amesema katika mahojiano na televisheni ya MSNBC kuwa Canada pia ipo tayari kulipiza kisasi katika uga huo wa ushuru iwapo Rais mteule wa Marekani Donald Trump atatekeleza nyongeza ya ushuru wa asilimia 25 kwa bidhaa kutoka Canada na Mexico. 

Trump pia ameitaja Canada kuwa jimbo la 51 la Marekani katika hali ambayo awali serikali ya Waziri Mkuu wa Canada ilichukulia suala hilo kama mzaha lakini sasa kadhia hii imepewa uzito maalumu. 

Rais mteule wa Marekani, Donald Trump

Trudeau amesema katika mahojiano hayo kuwa wanachi wa Canada wanapaswa kuyachukulia matamshi ya hayo ya kujitanua ya Trump kuwa suala la jadi. 

Wakati huo huo, Mélanie Joly, Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada amesema kuwa matamshi ya Trump yanaonyesha kuwa haelewi ni nini kitakachoibadilisha Canada na kuwa nchi yenye nguvu. Amesema uchumi wa Canada umeimarika, na watu wa nchi hiyo wako imara. 

Itakumbukwa kuwa Trump aliwahi kumwita Justin Trudeau kuwa Gavana wa jimbo kuu la Canada.

Trudeau alitangaza Jumatatu iliyopita kuwa ana nia ya kuachia ngazi baada ya kusalia kwa miaka tisa katika serikali ya kidemokrasia ya Chama cha Liberal, na kwamba ataendelea kushikilia wadhifa wake hadi hapo chama kitakapomteuwa mrithi wake.