UN yataka kuheshimiwa kikamilifu makubaliano ya kusimamisha vita Ghaza
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa mwito kwa pande zote kuheshimu kikamilifu makubaliano ya kusitisha mapigano huko Ghaza.
Antonio Guterres ametilia mkazo mkazo kuheshimiwa kikamilifu makubaliano ya kusimamisha vita Ghaza kwa kusema: "Hakuna kinachoweza kuhalalisha maafa ya vifo vya Wapalestina na uharibifu mkubwa uliosababishwa na Israel huko Ghaza."
Matamshi ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa yametolewa sambamba na tangazo la kufikiwa makubaliano ya kusimamisha vita huko Ghaza lililotolewa usiku wa kuamkia leo Alkhamisi.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Kizayuni, wafungwa 3 wa Kizayuni wamepangwa kuachiliwa huru na HAMAS siku ya kwanza, wafungwa 4 siku ya saba, wafungwa 3 siku ya kumi na nne,na wafungwa 3 zaidi wa Kizayuni wataachiliwa huru siku ya ishirini na moja. Siku ya ishirini na nane, wafungwa wengine watatu wa Kizayuni wataachiliwa na HAMAS, siku ya thelathini na tano, wafungwa wengine watatu na katika wiki ya mwisho, wafungwa wa Kizayuni waliosalia wataachiliwa.
Mkabala wa hatua hiyo ya HAMAS, katika awamu ya kwanza ya makubaliano hayo, karibu Wapalestina 1,000 waliotekwa nyara na Israel wataachiliwa huru.
Huko nyuma duru za Palestina na Israel zilitangaza kuwa utawala wa wa Kizayuni utawaachilia huru Wapalestina 200 waliohukumiwa kifungo cha maisha jela kama sehemu ya mazungumzo ya kubadilishana wafungwa na Hamas.
Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar, makubaliano hayo yamepangwa kuanza kutekelezwa rasmi siku ya Jumapili.