Russia: Magharibi inaudhoofisha Umoja wa Mataifa na kuuondolea itibari yake
https://parstoday.ir/sw/news/world-i121636-russia_magharibi_inaudhoofisha_umoja_wa_mataifa_na_kuuondolea_itibari_yake
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia ametahadharisha kuhusu vitendo vya Magharibi vinavyolenga kuudhoofisha Umoja wa Mataifa.
(last modified 2025-01-19T07:29:45+00:00 )
Jan 19, 2025 07:29 UTC
  • Russia: Magharibi inaudhoofisha Umoja wa Mataifa na kuuondolea itibari yake

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia ametahadharisha kuhusu vitendo vya Magharibi vinavyolenga kuudhoofisha Umoja wa Mataifa.

Maria Zakharova ameeleza katika taarifa na kuonya kwamba: "Magharibi sasa hivi inaudhoofisha na kuuondolea itibari Umoja wa Mataifa na unaliendeleza kwa msisitizo suala hili."
 
Inafaa kuashiria kuwa, Russia daima imekuwa ikipinga hatua za upande mmoja zinazochukuliwa na nchi za Magharibi dhidi ya nchi hiyo hususan kuhusu vikwazo dhidi yake kwa kisingizio cha vita vya Ukraine na imesisitizia umuhimu wa nafasi kuu ya Umoja wa Mataifa badala ya kujichukuliwa maamuzi ya upande mmoja.
 
Katika sehemu nyingine ya taarifa yake, Zakharova amekosoa makubaliano ya hivi karibuni ya Ushirikiano wa Miaka 100 yaliyosainiwa kati ya Ukraine na Uingereza, na kusema kuwa hayana umuhimu wowote.
 
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia amesisitiza kuwa, hakuna nafasi yoyote ya kuanzishwa ushirikiano kati ya Ukraine na Uingereza katika Bahari ya Azov na akabainisha kwamba makubaliano hayo ni mbinu ya kipropaganda tu inayotumiwa na serikali ya Ukraine.
 
Zakharova ameongezea kwa kusema: "Moscow itakabiliana vikali na madai yoyote kuhusu eneo la maji ya Bahari ya Azov."
 
Inafaa kuashiria kuwa Mkataba wa Ushirikiano wa Miaka 100 kati ya Ukraine na Uingereza ulitiwa saini siku ya Alkhamisi iliyopita wakati wa ziara ya Waziri Mkuu wa Uingereza Sir Keir Starmer nchini Ukraine.
 
Hati iliyotolewa baada ya kusainiwa makubaliano hayo inaonyesha kuwa kuna mipango kadhaa iliyoandaliwa kwa ajili ya kuanzisha vituo vya kijeshi nchini Ukraine na kushirikiana pande mbili za London na Kiev kwenye mifumo ya silaha za masafa marefu.../