Uchunguzi: Gen Z wanasumbuliwa na matatizo ya kiafya na kiakili
Utafiti mpya umegundua kuwa Kizazi cha Z (Generation Z) kinatatizika katika nyanja zote za maisha, na kinasumbuliwa na kuporomoka kwa kasi afya ya akili na mwili, hali ya kifedha na kijamii, na kukumbwa na mogoro wa mapema wa kipindi cha katiakati ya umri.
"Afya jumla" ya Gen Z imepungua kwa 6% tangu mwaka uliopita. Afya hiyo inafafanuliwa kuwa ni mchanganyiko wa afya ya akili, mwili, hali ya kifedha na kijamii.
Utafiti huo ambao umeripotiwa na Newsweek, ulifanywa mwezi Septemba na MetLife nchini Marekani na utachapishwa Machi 2025.
Kizazi Z (Gen Z) kinajumuisha watu waliozaliwa kati ya 1997 na 2012, ikimaanisha kuwa mwanachama mzee zaidi wa Generation Z atafikisha miaka 28 mwaka huu, na mdogo zaidi atakuwa na umri wa miaka 13.
Todd Katz, makamu mwenyekiti wa MetLife, ameiambia InsuranceNewsNet kwamba "Utafiti umeonyesha kuwa afya ya kundi hilo imepungua zaidi kuliko makundi mengine ya umri.
Utafiti huo pia unaonyesha kuwa 46% ya Kizazi Z wanasumbuliwa na mfadhaiko, 35% wanahisi huzuni, 44% wanahisi kuishiwa nguvu, na 30% wanajihisi kutengwa.
Utafiti mwingine umegundua kuwa 60% ya wanawake wa Gen Z na 45% ya wanaume wa kizazi hicho wanasmbuliwa na wasiwasi kwamba kupanda kwa gharama ya maisha kutazuia usalama wao wa kifedha katika siku zijazo.