CNN: Idadi ya wanajeshi wa Marekani waliouawa nchini Ukraine inaongezeka
Televisheni ya CNN ya Marekani imeripoti kuwa idadi ya wanajeshi wa Marekani waliouawa kwenye mstari wa mbele wa vita nchini Ukraine imeongezeka katika kipindi cha miezi 6 iliyopita.
CNN iliripoti jana Alhamisi kwamba miili ya Wamarekani wasiopungua watano ambao walikuwa wamejiandikisha katika jeshi la Ukraine imeachwa kwenye uwanja wa vita baada ya kuuawa na haikuweza kupatikana tena kutokana na mapigano makali.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, maiti za wawili kati ya wanajeshi wa Marekani waliouawa zimerejeshwa katika eneo la Ukraine kutoka maeneo ambayo sasa yanadhibitiwa na Russia baada ya mazungumzo marefu.
Manusura na jamaa wa wanajeshi wawili wanasema Wamarekani hao waliuawa katika operesheni nje ya mji wa Pokrovsk mashariki mwa Ukraine mwishoni mwa Septemba, na hakuna maiti iliyopatikana.
Ripoti ya CNN inasema kuwa wanajeshi 20 wa Marekani wametoweka nchini Ukraine kufikia sasa.
Vita vya Ukraine vilianza kutokana na nchi za Magharibi kupuuza wasiwasi wa usalama wa Moscow kuhusu upanuzi wa mipaka ya muungano wa kijeshi wa NATO (North Atlantic Treaty Organization).
Moscow iliivamia Ukraine mnamo Februari 2022 baada ya nchi za Magharibi, haswa Merekani, kupuuza wasiwasi wake wa usalama.